Wanachama wapya wakikabidhi kadi zao kwa Katibu wa Itikadi,Uenezi na Mafunzo Taifa CPA Amos Makala


Na Hellen Mtereko Mwanza
Katibu wa Itikadi,Uenezi na Mafunzo Taifa CPA Amos Makala, ameongoza zoezi la kuwapokea viongozi watano wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) pamoja na wanachama wapya kutoka vyama mbalimbali 165 Jijini Mwanza.
Zoezi hilo lilifanyika Jana Mei 02, 2025 kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya furahisha jijini hapa.
Wanachama hao wametaja sababu mbalimbali za kuhamia CCM ikiwemo kuridhishwa na utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Akizungumza mara baada ya kupokelewa Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Mwanza, Peter Matyoko alisema kauli ya ‘No reform no election’ imekuwa ikimuumiza sana na ndio maana akaamua kujiunga na CCM.
“Serikali yetu inatenda haki kwakila vyama na haina ubaguzi sasa inapofika viongozi wa chama kutaka kuzuia uchaguzi usifanyike kwakweli waliniathiri kisaikolojia nikaona nibora nijiunge na CCM ili uchaguzi utakapofika niweze kuchagua viongozi watakao tuletea maendeleo”, Alisema Matyoko
Naye Jacksoni James ambaye ni mwanachama mpya aliejiunga na CCM alisema amejiunga na chama hicho kwa hiari yake mwenyewe na yuko tayari kushirikiana na wengine kwaajili ya kukijenga chama.
Akizungumza mara baada ya kuwapokea wanachama hao CPA Makala amewapongeza wanachama hao kwa kuhamia CCM huku akitoa maelekezo kwa katibu wa Mkoa kuwaweka katika utaratibu na usajili mzuri kwani wanakwenda kuongeza idadi ya wanachama walioko kwenye Cha hicho.