Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele leo Mei 03, 2025 ametembelea na kukagua vituo vya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura awamu ya pili linalokwenda sambamba na uwekaji wazi wa daftari la awali la wapiga kura mkoani Ruvuma katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea na Halamashauri ya Namtumbo ambapo mikoa 15 inaendelea na zoezi hilo. Pichani ni Mwenyekiti wa Tume akiwa katika kituo cha Shule ya Msingi Litola iliyopo Wilayani Namtumbo. (Picha na INEC).