Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Dkt. Ashatu Kijaji amesema Serikali hivi karibuni itahitimisha mchakato wa ununuzi wa meli nane kwa ajili ya uvuvi wa bahari kuu.
Waziri Kijaji amesema hayo leo Mei 6, 2025 katika mkutano na waandishi wa habari kuelezea mafanikio ya Serikali ya awamu ya sita kwenye Wizara ya Mifugo na Uvuvi katika Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo Dodoma.
Meli hizo zitatumika kwa shughuli za uvuvi Tanzania Bara na Zanzibar, ambapo kwa upande wa Tanzania Bara, meli hizo zitatumiwa na Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO).
WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi Dkt.Ashatu Kijaji,akizungumza na Waandishi wa Habari leo Mei 6, 2025 jijini Dodoma kuhusu Mafanikio ya Wizara hiyo katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan.