Dar es Saalam .
Takukuru wilaya ya Ilala imefanikiwa kuokoa zaidi ya shs milioni 14 ambazo ni kodi ambayo awali ilikuwa haijalipwa baada ya kufanya ufuatiliaji kwenye miradi mbalimbali .
Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Takukuru Wilaya ya Ilala Sosthenes Kibwengo wakati akizungumza na waandishi wa habari .
“Katika utendaji kazi wetu tangu januari hadi machi 2025 tumetekeleza mambo mbalimbali ikiwemo uzuiaji rushwa .”
Amesema kuwa,katika eneo la uzuiaji rushwa wamefuatilia na kukagua miradi 12 ya maendeleo yenye thamani ya shs zaidi ya bilioni 10 katika sekta za ujenzi elimu afya biashara na utawala kwa lengo la kuhakikisha kwamba thamani halisi ya fedha na makusudio mazuri ya serikali yanatimilika.
Amesema kuwa ,kwa ujumla miradi mingi inaendelea vizuri na mapungufu machache yaliyobainika yamerekebishwa ingawa bado tuna tatizo la jumla la udhaifu katika.usimamizi ambao unaosababisha baadhi ya miradi kitekelezwa bila kuzingatiwa kwa vigezo na mikataba na baadhi ya miradi kuchelewa .
Ameongeza kuwa, ufuatiliaji huo umewezesha kuokoa zaidi ya shs milioni 14 ambazo ni kodi ambayo awali ilikuwa haijalipwa .
Amefafanua kuwa, wanafanya pia kazi za uchambuzi wa mifumo kwa lengo la kubaini mianya ya rushwa katika utendaji kazi au utoaji huduma wa sekta mbalimbali kwa kushirkiana na wadau wanajaribu kuitafutia utatuzi mianya hiyo ya rushwa .
Ameongeza kuwa, katika kipindi hicho wamefanya uchambuzi wa mifumo miwili ya utendaji kazi katika sekta ya mapato na ardhi .
Kibwengo amesema kuwa katika.uchambuzi wa mfumo wa mapato yatokanayo na maegesho ya vyombo vya usafiri katika halamshauri ya jiji la Dar es Salaam wamebaini kwamba kuna uwepo wa vituo vya bajaji na bodaboda ambavyo havijasaliwa au venye vifaa vya usafiri kwa idadi zaidi ya iliyoanishwa na hivyo kukosea Halmashauri mapato .
Amefafanua kuwa,kuna udhaifu katika kusimamia mikataba ya maegesho kati ya halmashauri. Na wawekezaji mbalimbali.na hivyo kusababisha kutokusanywa kikamilifu kwa ada za maegesho na kukosesha halmashauri mapato.
Aidha amesema kuwa wamebaini wakusanya mapato baadhi yao kutoa risiti zisizo na namba ya usajili wa chombo husika cha usafiri pamoja na kuwepokwa upungufu wa mashine za kukusanya mapato na hivyo kukwamisha ukusanyaji wa ada za maegesho .
“Pamoja na kuwa tumekaa na kukubaliana na halmashauri ya jiji la Dar es Saalam namna bora ya kuondokana na mapungufu hayo uchunguzi wetu umebaini kumekuwa na kuimarika kwa mapato kwa asilimia 55 katika eneo la shule moja ya sekondari baada ya halmashauri ya jiji kuanza kukusanya ada katika eneo hilo yenyewe. “amesema .
Amefafanua kuwa, wamebaini pia kutokuwepo kwa usimamizi usioridhisha kwa maeneo ya wazi kwa kutokuwepo alama za mipaka na mawasiliano hafifu kati ya idara ya mipango miji na halmashauri ya jiji la Dar es Saalam na ofisi za kata na hivyo kuwezesha wananchi ambao hawana nia njema kuvamia maeneo hayo katika maeneo yanayotengwa kwa shughuli za kiserikali ambayo ni maeneo ya wazi hivyo kuna watu wamebaini kuvamia maeneo hayo.
Aidha ametoa wito wote waliovamia maeneo ya wazi katika halmashauri ya jiji la Dar es Salaam kuachi mara moja kwani wanafuatilia na mkono wa Sheria utawafikia .