Wakazi wa Zanzibar wakipata elimu kuhusu huduma za upasuaji wa moyo zinavyofanyika katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kutoka kwa Afisa Uuguzi wa Taasisi hiyo Edna Kajuna wakati wa maonesho ya Wiki ya Afya Zanzibar yanayoendelea katika viwanja vya Golden Tulip Airport Zanzibar.
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Shirika lisilo la kiserikali Heart Team Africa Foundation (HTAF) Linda Gideon akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa timu ya mpira wa miguu Young African (Yanga) mara baada ya kuchangia matibabu ya upasuaji wa moyo kwa watoto kwa kununua T-shirt wakati wa maonesho ya Wiki ya Afya Zanzibar yanayoendelea katika viwanja vya Golden Tulip Airport Zanzibar
Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Edna Kajuna akimuonesho mtangazaji wa Clouds Tv Babuu wa Kitaa betri ya moyo (Pace maker) inayowekwa kwa wagonjwa ambao mapigo yao ya moyo yapo chini ya 50 wakati wa maonesho ya Wiki ya Afya Zanzibar yanayoendelea katika viwanja vya Golden Tulip Airport Zanzibar.
Wadau kutoka Zanzibar wakionesha bidhaa walizonunua kutoka Shirika lisilo la kiserikali Heart Team Africa Foundation (HTAF) kwaajili ya kuchangia upasuaji wa moyo kwa watoto wanaotibiwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI). – Picha na: JKCI