Na MWANDISHI WETU,Tanga.
Wajumbe wa Baraza Kuu la 54 la Wafanyakazi wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), wakiongozwa na Mkurugenzi Mkuu, Bw. Masha Mshomba wamepatiwa mafunzo mbalimbali yaliyolenga kuongeza uelewa wa huduma wanazozipata kutoka NHIF, PSSSF, RITA, Kampuni Tanzu ya NSSF, Sisalana pamoja na elimu kuhusu afya ya akili.
Mafunzo hayo yamefanyika tarehe 7 Mei 2025, ikiwa ni maandalizi ya kuelekea Mkutano wa 54 wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Mfuko unaofanyika jijini Tanga wenye lengo la kujadili Mpango na Bajeti ya Mfuko kwa mwaka wa fedha 2025/26.