•Akiri kupokea changamoto za barabara, Maji, Umeme na maombi ya hospitali ya Wilaya ya Ulanga
ULANGA: Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, CPA Amos Makalla amesema pamoja na mafanikio ya miradi mingi ya maendeleo amepokea changamoto za barabara, miradii maji kuchelewa, mawasiliano na kukatiika katika kwa umeme kwenye Wilaya ya Ulanga Malinyi
Pia amesema anakiri kupokea changamoto zilizopo ikiwemo barabara, maji umeme na maombi ya hospitali ya Wilaya Ulanga kwa kuwataka mawaziri wa wizara husika kufika ili kutatua changamoto hizo.
Makalla ameeleza hayo leo Mei 9, wakati akizungumza na wananchi katika Kata ya lupiro waliojumuisha Wilaya ya Mbili ya Ulanga na Malinyi mkoani Morogoro ikiwa ni muendelezo wa ziara ya siku saba mkoani humo.
Makalla amesema serikali ina nia nzuri kwa wananchi wake na mendeleo yanayofanyika ni ushahidi dhahiri kuonesha nia hiyo na yeye amepita katika ziara zake kusafisha njia ili Rais, Waziri Mkuu na viongozi wengine waweze kupita kwa ajili ya kuendelea na utatuzi wa changamoto za wananchi.
Aidha Makalla amesema anatambua kuna changamoto za barabara kutoka Kilombero hadi Mahenge lakini amefanya mawasiliano na Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega aweze kufika ili kuweza kutatua changamoto hiyo akiwa kama msaidizi wa rais kwenye ujenzi wa barabara.
Amesema katika upande wa maji amefanya mawasiliano na Waziri wa Maji, Juma Aweso aweze kufika kutatua changamoto hiyo na kuhusu umeme alisema upo lakini ni wa kusus sua na atafanya mawasiliano na Waziri wa Nishati kuona namna ya kutatua hilo.
Sambamba na hayo Makalla amesema Mkoa wa Morogoro ni matajiri kwa shughuli mbalimbali za kiuchumi ikiwemo kilimo cha mazao ya chakula na biashara na kwakulitambua hilo Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa akitoa fedha kwa ajili ya kuendeleza miradi mbalimbali ya kilimo katika mkoani humo.
“Mkoa wa Morogoro ni ghala la chakula miradi mbalimbali ya kilimo, ikiwemo umwagiliaji Rais Samia ameendelea kumwaga fedha kuhakikisha miradi hiyo inatekelezwa na kurndelea kuiilinda ili kukuza uzalishaji,” amesema Makalla.
Aidha, Makalla amewataka wananchi kuendelea kusimama na muunga mkono Rais Samia katika kulinda amani, na kusisitiza vijana wasikubali kutumika na wanasiasa katika uvunjifu wowote wa amani.