Na Mwandishi Wetu
Mariam ameyasema hayo wakati akizungumza na Wananchi wa Kata ya Msanga wilayani Kisarawe mkoani Pwani ambapo amesisitiza ni vema wakahakiki majina yao katika daftari la mpiga kura pindi uhakiki awamu ya pili utakapoanza.
“Pia wale wananchi ambao wametimiza miaka 18 mwaka huu tunawahimiza kujiandikisha katika daftari la Kudumu la mpiga kura ili wakati wa uchaguzi mkuu utakapofika wapate haki yao kikatiba kichagua viongozi kwa maslahi ya Taifa letu.”

Mariam amesema kuwa masuala ukatili wa watoto yamekuwa ni mengi hivyo lazima wazazi kuwa sehemu ya walinzi watoto hao huku akieleza hivi sasa hata wanaume nao wanapigwa na wake zao na huo nao ni ukatilii, hivyo ametoa rai kwa wanawake waache kuwapiga waume zao na kuendelea na maisha ya amani.