Dar es Saaalam.
Shirika la Posta Tanzania limeshiriki katika kongamano la kimataifa la mkutano wa elimu mtandao kwa lengo la kutoa elimu na huduma mbalimbali zinazotolewa na shirika hilo.
Kaimu Meneja mauzo wa Shirika la posta Tanzania ,Andrew Liundi amesema kuwa wapo hapo kwa ajili ya kutoa huduma zake za kimkakati.
“Tupo hapo kwa ajili ya kutoa huduma zake za kimkakati kwa mujibu wa jukumu ambalo shirika limekasimiwa na serikali .”amesema .
Katika huduma hizo wamekuja kutoa huduma za usafirishaji maana wapo kwa ajili ya kuwahudumia wageni na wenyeji ili wakinunua chochote ndani ya kongamano hilo .
“Kuna waonyeshaji wa bidhaa mbalimbali hapa na tuna duka letu mtandaoni wanaweza kutembelea wakapenda wakanunua wakishanunia sisi tunawasafirishia popote pale ndani ama nje ya nchi .”amesema Liundi.
Amesema kuwa, wapo hapa kwa ajili ya kuleta huduma ya kubadilisha fedha lengo kuu la shirika ni kuondoa changamoto ya wageni ambao wanaweza kuja hapa wkaiwa na hela zao za kigeni na wanahitaji fedha za kitanzania katika kufanya miamala yao mbalimbali ili kuwaondolea adha ya kwenda pembezoni mwa mji na kukutana na wajanja wajanja au wakapata rate ambazo kimsingi sio rate rasmi zilizopo kwenye soko la fedha hivyo shirika lipo hapo kwa ajili ya kutoa huduma hiyo.
Aidha amefafanua zaidi kuwa, kuhusu hiyo Swift app ni huduma katika huduma zetu mama za usafirishaji na ni huduma itwa task mtandao kwa maana kuwa sasa hivi ndani shirika la posta unaenda kuita usafirishaji au chombo chetu kwa ajili ya kuja kubeba kifurushi au mzigo wowote ule kutola nyumbani hadi ofisini kwa kutumia control no ukalipa ukiwa umekaa nyumbani sio lazima ufike ofisini kwetu.
Amefafanua kuwa,wameenda mbali zaidi kuwa sasa unaweza kusafiri kutoka sehemu.moja kwenda nyingine kwa kutumia.huduma hiyo hiyo hata pembezoni mwa mji unaita kupitia hiyo tax mtandao ili uweze kusafiri wewe kama abiria na bei zake ni rafiki kabisa.
Aidha amefafanua zaidi kuwa,bei zao zimeangalia hali ya maisha ya watanzania ,hivyo amewataka kutoa huduma za posta za Tanzania hasa katika hizo huduma hizo alizotaja kwani ni huduma ambazo unaweza kutumia hata kama huna mtandao .
Huduma hii ipo nchi nzima sio mijini tu ipo mpaka mikoani kote na sio lazima uwe na bando lengo uwe tu simu janja unadaload app na kujisajili