RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwasalimia na kuwapongeza Wanafunzi wa Skuli za Msingi kutoka Mkoa wa Kusini Pemba, baada ya kumaliza kutowa burudani ya wimbo maalumu wa Uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa wa Msaada wa Kisheria ya Mama Samia, uzinduzi huo uliyofanyika Mkoa wa Kusini Unguja katika viwanja vya Mtende leo 10-5-2025.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Viongozi mbalimbali alipowasili katika viwanja vya Mtende Mkoa wa Kusini Unguja, kwa ajili ya uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia, uliofanyika leo 10-5-2025 Mkoa wa Kusini Unguja.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Divisheni ya Usimamizi Msaada wa Kisheria Zanzibar,Yusfa Abdalla Said, wakati akitembelea maonesho hayo yaliyofanyika katika viwanja vya Mtende Mkoa wa Kusini Unguja, kabla ya kuzindua Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia, uliyofanyika leo 10-5-2025 (kushoto kwa Rais) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria,Utumishi na Utawala Bora Zanzibar Mhe.Haroun Ali Suleiman.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akipata maelezo kutoka kwa Afisa wa Wizara ya Katiba na Sheria Tanzania –URT. Edith Shekidele, wakati akitembelea maonesho hayo yaliyofanyika katika viwanja vya Mtende Mkoa wa Kusini Unguja, kabla ya kuzindua Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia, uliofanyika leo 10-5-2025 (kushoto kwa Rais) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria,Utumishi na Utawala Bora Zanzibar Mhe.Haroun Ali Suleiman.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akipata maelezo kutoka kwa Mkaguzi wa Msaidizi wa Polisi, Vicent Innocent, Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto, wakati akitembelea maonesho hayo yaliyofanyika katika viwanja vya Mtende Mkoa wa Kusini Unguja, kabla ya kuzindua Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia, uliofanyika leo 10-5-2025 (kushoto kwa Rais) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria,Utumishi na Utawala Bora Zanzibar Mhe.Haroun Ali Suleiman.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akipata maelezo kutoka kwa Afisa Habari Kamisheni ya Wakfu na Mali ya Amana Zanzibar Asha Maulid Ali, wakati akitembelea maonesho hayo yaliyofanyika katika viwanja vya Mtende Mkoa wa Kusini Unguja, kabla ya kuzindua Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia, uliofanyika leo 10-5-2025 (kushoto kwa Rais) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria,Utumishi na Utawala Bora Zanzibar Mhe.Haroun Ali Suleiman.(Picha na Ikulu)
WANANCHI wa Mkoa wa Kusini Unguja wakifuatilia hutuba ya ufunguzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia, wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akihutubia na kuifungua kampeni hiyo iliyofanyika katika Mkoa wa Kusini Unguja leo 10-5-2025. Katika viwanja vya Mtende.(Picha na Ikulu)
BAADHI ya Wanasheria wakifuatilia hafla ya Uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia, uzinduzi huo uliyofanyika katika viwanja vya Mtende Mkoa wa Kusini Unguja leo 10-5-2025.(Picha na Ikulu)
BAADHI ya Viongozi mbalimbali wakifuatilia hutuba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) wakati akihutubia na kuzindua Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia, uzinduzi huo uliyofanyika leo 10-5-2025 katika viwanja vya Mtende Mkoa wa Kusini Unguja.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akihutubia na kuzindua Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia, uzinduzi huo uliyofanyika leo 10-5-2025 katika viwanja vya Mtende Mkoa wa Kusini Unguja.(Picha na Ikulu)