Fensi ya umeme ya majaribio iliyotengenezwa na shirika lisilo la kiserikali la Grumeti fund inatajwa kusaidia katika vijiji vinavyozunguka mapori ya akiba ya ikorongo na Grumeti ambapo wadau wa uhifadhi na utalii wameiomba serikali kuangalia namna ya kuweka fensi hiyo ya umeme katika maeneo ambayo yanakabiliwa na migogoro pamoja na wanyama wakali ili kuondoa changamoto hiyo ambayo imekuwa ikiepelekea serikali kulipa kifuta machozi mara kwa mara.
Kauli hiyo imetolewa na wadau wa uhifadhi kutoka katika mapori ya Burigi chato ,minziro mkoani kagera mara baada ya kutembelea na kujionea uwepo wa fensi hiyo ya umeme ilivyosaidia kupunguza mwilingiliano wawanyama katika maeneo hayo na kusababisha uharibifu mkubwa wa mazao pamoja na mauaji kwa binadamu.
Meneja mkuu wa shirika lisilo la kiserikali la Grumeti fund utafiti na jamii Bwana Noel Mbise alisema kwa sasa matukio na migogoro na wananchi imepungua katika maeneo hayo kufutia fensi ambayo inataribani km 30 imejengwa katika maeneo ya park nyigoti,miseke na vijiji vingine ambavyo vinazuguka pori hilo upande wa Serengeti.
“ Unaona katika maeneo haya malalalamiko yamepungua na usalama upo lakini pia hata usalama wawanafunzi na wanyama kwa sasa nimkubwa maana mnyama hususani tembo anapotaka kuvuka akipigwa shoti anarudi kwahiyo anaendelea kua salama mnyama pamoja na mkazi ambaye yuko upande wa pili nae anaendelea kuwa salama kwahiyo nijambo la kujivunia”Alisem noel Mbise meneja mkuu Grumeti fund utafiti na jamii.
Kwa upande wake mhifadhi mwandamizi katika hifadhi ya Taifa ya Burigi Chato Ombeni Higi amesema amejifunza kwa sehemu kubwa kuhusisna na fensi hiyo kutokana na hifadhi ya Burigi kumekuwa na matukio mengi ya tembo hivyo kama njia hiyo itatumika itasaidia kupunguza migogoro baina ya hifadhi na wanayama.
Aidha naye Bwana Michael Kimaro ambaye nimkurugenzi mtendaji kutoka taasisi isiyi ya kiserikali Tanzania Reseach and Conevetion TRC alisema kuanzishwa kwa fesni hiyo ya umeme ilikuwa na lengo la kufanya majaribio kuangaliana namna ya kutoa msaada dhidi ya wanayama na sasa imeonesha matokeo chanya hivyo serikali iangalie namna ya kuweka kwenye maeneo ya wananchi ili kuondoa migogoro inayojitokeza.