Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwa na Mwenza wake Mama Mbonimpaye Mpango wakiwasili katika viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam kushiriki kuaga mwili wa aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais Mstaafu na Waziri Mkuu Mstaafu hayati Cleopa David Msuya. Tarehe 11 Mei 2025.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwa na Mwenza wake Mama Mbonimpaye Mpango akisaini kitabu cha maombolezo mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam kushiriki kuaga mwili wa aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais Mstaafu na Waziri Mkuu Mstaafu hayati Cleopa David Msuya. Tarehe 11 Mei 2025.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akishiriki kuaga mwili wa aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais Mstaafu na Waziri Mkuu Mstaafu hayati Cleopa David Msuya katika viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam tarehe 11 Mei 2025.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akizungumza wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais Mstaafu na Waziri Mkuu Mstaafu hayati Cleopa David Msuya katika viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam tarehe 11 Mei 2025.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwa na Mwenza wake Mama Mbonimpaye Mpango wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais Mstaafu na Waziri Mkuu Mstaafu hayati Cleopa David Msuya katika viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam tarehe 11 Mei 2025.
…………
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango ameungana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Viongozi mbalimbali, familia pamoja na waombolezaji mbalimbali katika Ibada ya kuaga na kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Makamu wa Kwanza mstaafu na Waziri Mkuu mstaafu hayati Cleopa David Msuya iliyofanyika katika viwanja vya Karimjee Jijini Dar es salaam.
Akizungumza katika tukio hilo, Makamu wa Rais amesema hayati Cleopa David Msuya katika utumishi wake Serikalini alikuwa mzalendo, mwadilifu na mchapakazi mahiri. Amesema Kiongozi huyo ni mfano bora wa kuigwa na Serikali inathamini uzalendo na mchango wake mkubwa katika maendeleo ya Taifa.
Pia Makamu wa Rais amesema hayati Cleopa David Msuya katika maisha baada ya kustaafu, alikuwa kisima cha busara na marejeo ya kumbukumbu katika Taifa pamoja na kuwa mfuatiliaji makini wa mambo. Ameongeza kwamba kiongozi huyo alikuwa mchambuzi hodari wa mambo,mkweli na mwenye msimamo thabiti.
Makamu wa Rais amesema hayati Cleopa David Msuya aliendelea kufuatilia utatuzi wa changamoto za maendeleo za wananchi wenzake wa Mwanga kila alipopata nafasi ya kusalimiana na viongozi wa Kitaifa wa sasa huku akitolea mfano alipomweleza kuhusu kusuasua kwa ukamilishaji wa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Mwanga na mradi wa maji wa Same – Mwanga – Korogwe, ambao umekamilika mwaka huu baada ya takriban miongo miwili ya utekelezaji.
Makamu wa Rais ametoa pole kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Familia na Wananchi wote kwa ujumla kufuatia msiba huo ambao ni pigo kubwa. Ameisihi familia kufarijika kwa kuwa hayati Cleopa David Msuya ataendelea kuwa katika historia ya Tanzania kama kiongozi wa kipekee aliyeacha alama. Pia amewaomba wanafamilia kukamilisha uandishi wa kitabu kuhusu maisha ya hayati Msuya ambacho kilikuwa karibu kukamilika.