Na Mwandishi Wetu
Mkurugezi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF Shadrack Mziray amelishukuru Shirika la Chakula Duniani kwa Niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa Mchango wao wanaoutoa wa kunusuru kaya Masikini.
Amesema Shirika hilo la Chakula lina mchango mkubwa katika miradi ya maendeleo ya Wananchi hali inayowasaidia kujikomboa na umasikini na kufanya miradi ya maendeleo.
Mziray amezitoa pongezi wakati wa kikao cha majadiliano kuhusu mpango mpya wa TASAF awamu ya Tatu unaotarajiwa kuaza Oktoba mwaka huu.
Amesema katika kikao hicho Shirika la Chakula Duniani limekubali kuendelea kushirikiana na Serikali katika utekelezaji wa mpango mpya wa kunusuru kaya masikini.
Mkurugezi WPF Tanzania Ronald Tranbahuy amesema shirika hilo limeridhishwa na muendelezo katika miradi na uwezeshaji wananchi kiuchumi.
Wakati awamu ya Pili ya Mpango wa kunusuru kaya Masikini ukitarajia kumalizia Septemba nakuaza kwa awamu ya Tatu Oktoba mwaka huu .Wadau wa Maendeleo wamekua na ziara mbali mbali za tathimini ya kawaida ya kuangalia Maendeleo ya utekelezaji wa mpango wa TASAF.
