UMOJA wa Haki ya Kupata Taarifa (CoRI) umekutana ilikujadili mambo matatu muhimu ikiwemo kusaini makubaliano yatakayosaidia umoja huo ikiwa ni kuelekea uchaguzi Mkuu wa 2025.
Makubaliano hayo yanatokana na mkakati waliojiwekea kwa kipindi cha miaka minne na tatu ni namna gani ujumbe wa CoRI utafika kwa jamii
Akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya kuhitimisha kikao na wanachama wa CoRI leoMei 12,2025, Dar es salaam Mwenyekiti wa CoRI, Ernest Sungura amesema Umoja huo unalenga kukuza uhuru wa vyombo vya habari pamoja na uwajibikaji wake.
Amesema vipaumbele walivyozungumziwa na CoRI ni juu ya usalama wa waandishi wa habari ikiwa ni kuelekea uchaguzi Mkuu.
“Sisi tutasimamia suala la usalama wa waandishi wa habari, miundombinu mbinu rafiki itakayosaidia utendaji kazi mzuri pamoja na usimamizi wa sheria za uchaguzi zilizowekwa na tume huru ya uchaguzi zikiwataka wasimamizi kutoa taarifa kwa waandishi wa habari kabla ya mamlaka husika”amesema Sungura.
Sungura amesema umoja huo hautapoa katika kupigania haki za waandishi wa habari ambayo ni haki ya kupata taarifa kwani mwandishi asipopata taarifa kwa ajili ya kuhabarisha umma hakutakuwa na vyombo vya habari.
Amesema katika kuelekea uchaguzi Mkuu utakao fanyika mwezi Oktoba mwaka huu, wanachama wa CoRI tayari wamekwisha anza kutoa mafunzo kwa Waandishi wa Habari lakini pia wapi katika maandalizi ya kutoa vitendea kazi vitakavyotumika wakati wa kutoa taarifa za uchaguzi huo.
Kwa sasa CoRI ina jumla ya wanachama 16 ambao ni Baraza la Habari Tanzania (MCT), Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika Tawi la Tanzania (MISA-TAN), Chama cha Wanawake Wanahabari Tanzania (TAMWA), Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT), Ofisi ya Habari kwa Wananchi wa Tanzania (TCIB), Sikika, Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), JamiAfrica, Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Twaweza, OJADACT, Policy Forum, Shirika la Maendeleo na Habari Tanzania (TADIO), Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC).