Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Said Mtanda (wapili kulia) akikagua nyavu za usalama chini ya ardhi zinazotengenezwa na kampuni ya Rock Solutions Limited.

Meneja wa Kampuni ya Rock Solutions Fabiani Mayenga akitoa taarifa ya kiwanda.




………….
Na Hellen Mtereko, Mwanza
Katika kuunga mkono juhudi za Serikali za upatikanaji wa ajira nchini Kampuni ya Rock Solutions Limited imeanzisha kiwanda cha kuzalisha nyavu za usalama chini ya ardhi (Wire mesh for underground support)ambacho kinatarajiwa kuzalisha ajira za moja kwa moja 300 huku wananchi zaidi ya 500 kunufaika kupitia uwekezaji huo.
kiwanda hicho kipo Wilaya ya Misungwi,Tarafa ya Usagara Kijiji cha Kaluluma Mkoani Mwanza.
Hayo yamebainishwa na Meneja wa Kiwanda cha Rock Solution, Fabiani Mayenga wakati alipokuwa akitoa tarifa ya kiwanda hicho.
Alisema kiwanda hicho kimejikita katika kuzalisha vifaa vinavyotumika kwenye migodi ikiwemo nyavu zinazotumika kuzuia maporomoko ya ardhi chini ya migodi.
“Kiwanda hiki kitakapokamilika kitagharimu bilioni 4.7 kwa sasa tupo kwenye hatua ya kufunga mashine na mitambo mbalimbali tunatarajia kazi hii itakamilika mwishoni mwa mwezi wa tano mwaka huu”, Alisema Mayenga
Aidha, aliongeza kuwa uwepo wa kiwanda hicho ni chachu ya maendeleo na ukuaji wa uchumi katika maeneo husika na taifa kwa ujumla.
Akizungumza mara baada ya kukagua kiwanda hicho Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Said Mtanda, alisema Serikali itaendelea kushirikiana na sekta binafsi kwani wanatambua mchango wao wa kusaidia kupunguza wimbi la ukosefu wa ajira.