Mkurugenzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Ramadhani Kailima (kushoto), akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Adam Malima, baada ya mazungumzo kati ya INEC na Mkuu wa Mkoa huyo kuhusu uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura awamu ya pili linalokwenda sambamba na uwekaji wazi wa Daftari la Awali la Wapiga Kura, linalotarajiwa kuanza Mei 16 hadi 22 Mkoani Morogoro, yaliyofanyika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mjini Morogoro leo Mei 14, 2025. Katikati ni Mjumbe wa INEC, Mhe. Balozi Omar Mapuri. Picha na INEC
Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe. Balozi Omar Mapuri (kushoto), akisalimiana na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume hiyo, Ramadhani Kailima wakati akiwasili Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro leo Mei 14, 2025, kwa ajili ya mazungumzo kati ya INEC na Mkuu wa Mkoa kuhusu uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura awamu ya pili linalokwenda sambamba na uwekaji wazi wa Daftari la Awali la Wapiga Kura, linalotarajiwa kuanza Mei 16 hadi 22 Mkoani Morogoro. Picha na INEC.
Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Balozi Omar Mapuri (kushoto), akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Adam Malima, baada ya mazungumzo kati ya INEC na Mkuu wa Mkoa huyo kuhusu uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura awamu ya pili linalokwenda sambamba na uwekaji wazi wa Daftari la Awali la Wapiga Kura, linalotarajiwa kuanza Mei 16 hadi 22 Mkoani Morogoro, yaliyofanyika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mjini Morogoro leo Mei 14, 2025. Picha na INEC.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Adam Malima akizungumza na Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Balozi Omar Mapuri (Katikati) na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume hiyo, Ramadhani Kailima (kushoto), kuhusu uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura awamu ya pili, katika kikao kilichofanyika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, mjini Morogoro, leo Mei 14, 2025. Picha na INEC