WAZIRI wa Viwanda na Biashara Mhe.Dkt.Selemani Jafo ,akizungumza na Waandishi wa Habari leo Mei 15,2025 jijini Dodoma kuhusu Mafanikio ya Wizara hiyo katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan.
WAZIRI wa Viwanda na Biashara Mhe.Dkt.Selemani Jafo ,akizungumza na Waandishi wa Habari leo Mei 15,2025 jijini Dodoma kuhusu Mafanikio ya Wizara hiyo katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan
Na.Alex Sonna_DODOMA
WIZARA ya Viwanda na Biashara imetaja mafanikio iliyopata katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita ikiwemo kuongezeka kwa Viwanda ambavyo vimeongeza ajira kwa watanzania.
Kauli hiyo imetolewa leo Mei 15,2025 Jijini Dodoma na Waziri wa Wizara hiyo,Mhe.Dkt.Selemani Jafo wakati akieleza mafanikio ya miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita.
Waziri Jafo amesema katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita, Viwanda vimekuwa vingi ambavyo vimetoa fursa ya ajira na kuongeza Pato la Taifa.
Amesema uwepo wa kiwanda cha Makaa ya Mawe kumeongeza ajira kwa watanzania na Serikali imefungua bandari ya Mtwara kwa ajili ya kusafirisha makaa ya mawe.
“Mradi wa Katewaka utasaidia kupata ajira kwa vijana.Niwapongeze NDC kwa kusimamia hili.Baba wa Taifa Nchi yetu aliigawanya kwa kuwa na Viwanda vingi,Mwanza,Tanga,Morogoro na mwendelezo umekuwa ni mzuri,”amesema Waziri Jafo.
Amesema uwepo wa Viwanda vya Sukari,mbolea na kuwa na eneo maalumu la Kwala ambalo kuna Viwanda vingi kumezidi kufungua fursa za ajira.
Amesema wamefanikiwa katika uzalishaji wa bidhaa muhimu ikiwemo uunganishaji wa vifaa vya magari na Kuna Viwanda 15.
Amesema Viwanda hivyo uzalishaji wake ni mkubwa na ajira za wazawa ni nyingi kuliko wageni wanaotoka nje.
“Ni mafanikio makubwa mno.Niwaombe watanzania tuwe wazalendo na hii ni kazi kubwa inayofanywa na Rais.
Kwenye Viwanda vya vioo,Waziri Jafo amesema kwa sasa Tanzania ina Viwanda vinne ambapo Imani ya Serikali kwamba imeishajitosheleza.
“Imani yetu tutaungana pamoja tutumie mali zetu kwa kununua Viwanda,soko letu tunapeleka mpaka nje ya Bara la Afrika haya ni Mapinduzi makubwa,”amesema
Amesema kwa sasa Tanzania ina Viwanda vitatu vya Marumaru ambavyo vimekuwa vikihakilisha mahitaji ya ndani anajitosheleza.
“Nchi yetu imeanza kujitosheleza kwenye kila kitu ndio maana Nchi zingine zinaagiza,”amesema Waziri Jafo