Na Janeth Raphael MichuziTv -Bungeni Dodoma
KATIKA mwaka wa fedha 2025/2026, Wizara ya Viwanda na Biashara kupitia idara ya maendeleo ya viwanda imepanga Kukamilisha marejeo na kutekeleza Sera Endelevu ya Maendeleo ya Viwanda pamoja na kuandaa Mpango Kabambe wa Maendeleo ya Viwanda
Hayo yameelezwa leo Mei 14,2025 bungeni na Waziri wa Wizara hiyo,Selemani Jafo wakati akiwasilisha bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2025-2026.
Ameyataja mambo mengine ni Kufanya mapitio ya Mkakati wa Ngozi na Mafuta ya Kula; Kuandaa Mpango Kabambe wa Maendeleo ya Viwanda;Kufanya Mapitio ya Sheria ya Chuma Chakavu; na Kuandaa Mkakati na Muongozo wa kuunda na kunganisha magari.
Pia amesema NDC imepanga Kuendelea na utekelezaji wa miradi ya kielelezo ya Mchuchuma, Liganga na mradi wa Magadi Soda Engaruka; Kuendelea kusimamia utekelezaji wa miradi ya Kimkakati ya Chuma Maganga Matitu, Makaa ya mawe Katewaka; Makaa ya Mawe Mhukuru pamoja na kulipia leseni za uchimbaji.
Vilevile Kuboresha utendaji wa kiwanda cha KMTC ,Kuboresha kiwanda cha Tanzania Biotec Limited kwa kuongeza uzalishaji wa bidhaa ya viuatilifu hai na Mbolea hai na kukamilisha upatikanaji wa Ithibati ya Ubora wa Kimataifa,Kuendelea na ufufuaji wa kiwanda cha Mang’ula.
Pia, Kuendelea na uboreshaji wa miundombinu katika Kongani ya TAMCO na Kange pamoja na kuendeleza eneo la Viwanda la Kimanjaro Machine Tools ili kuvutia wawekezaji Zaidi, Kuendeleza mashamba ya miti ya mpira kwa ajili ya kuzalisha malighafi viwanda na kutunza mazingira,
Vilevile Kuendelea na uboreshaji wa miundombinu ya Shirika ikiwemo ukarabati wa majengo na ofisi, na Kuboresha mfumo wa kitaasisi kwa kuimirisha mifumo ya kisheria, technolojia na kujenga ubobezi wa wataalamu wa shirika.