RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Viongozi mbalimbali wa Dini ya Kiislamu alipowasili Masjid Jibril Fuoni Bwiti Wilaya ya Magharibi “B” Unguja leo 16-5-2025 kwa ajili ya ufunguzi wa msikiti huo, na kujumuia na Wananchi katika Sala ya Ijumaa.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akikata utepe kufungua Masjid Jibril Fuoni Bwiti Wilaya ya Magharibi “B” Unguja, ufunguzi huo uliyofanyika leo 16-5-2025 na (kulia kwa Rais) Naibu Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Mahmoud Mussa Wadi na (kushoto kwa Rais) Mwenyekiti wa Jumuiya ya “Tears of Joy Foundation” Jaffar Hussein Babu na Sheikh Suwed Ali Suwed.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akikabidhiwa zawadi maalumu ya Msahafu na Sheikh Mohamed Omar Alsheikh Juda, wakati wa hafla ya ufunguzi wa Masjid Jibril Fuoni Bwiti Wilaya ya Magharibi “B” Unguja, ufunguzi huo uliyofanyika leo 16-5-2025.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na kuwasalimia Wananchi baada ya kumalizika kwa Sala ya Ijumaa iliyofanyika katika Masjid Jibril Fuoni Bwiti, baada ya kuufungua msikiti huo leo 16-5-2025.(Picha na Ikulu)
MUFTI Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi akizungumza kabla ya kumkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi kuzungumza na Waumini baada ya Sala ya Ijuma iliyofanyika katika Masjid Jibril baada ya kufunguliwa leo 16-5-2025.(Picha na Ikulu)