Waziri wa Ardhi Nyumba na maendeleo ya Makazi,Deogratius Ndejembi akizungumza kwenye mkutano huo jijini Arusha .



Happy Lazaro,Arusha .
Arusha .Waziri wa Ardhi Nyumba na maendeleo ya Makazi,Deogratius Ndejembi amesema serikali inaendelea na jitihada za kuwepo kwa kitengo cha miliki na kutunga sheria ya miliki ambayo pamoja na mambo mengine inategemea kuanzisha mamlaka ya kusimamia sekta ya miliki” real Estate”.
Aidha amesema kuwa,inaendelea pia na mkakati wa kuboresha sera ya nyumba na makazi ,ili kuendana na mabadiliko ya kijamii na kiuchumi ikiwemo ongezeko la watu na mahitaji ya makazi bora lengo likiwa ni kuwa na sera moja jumuishi itakayowezesha uundaji, usimamizi na uendelezaji wa sekta hiyo.
Ameyasema hayo Jijini Arusha wakati akifungua mkutano wa Tano wa chama Cha wataalamu wa miliki kuu Tanzania pamoja na kongamano la mwaka 2025 la jumuiya ya wataalamu wa miliki Afrika Mashariki unaoendelea jijini Arusha .
Amesema kuwa ,serikali pia itaunda sera na kutambua mchango wa sekta ya miliki katika ukuaji wa uchumi na Pato la Taifa hivyo itaweka utaratibu wa kusimamia kuendeleza, na kuthibiti sekta ya miliki .
Ndejembi amewataka pia wataalam wote wa nchi na Kanda ya Afrika ya Mashariki kuhakikisha wanadumisha maadili ya kazi kuheshimu miiko,taaluma zao kuendeleza ushirikiano wa taaluma ndani na nje ya nchi,kwani ushirikiano huo ndio utakaoifanya Afrika Mashariki kuwa kitovu cha maendeleo.
“serikali itaendelea kuratibu na kusimamia kuendeleza sekta hiyo nchini ili kuhakikisha haki za wadau zinalindwa na taaluma hiyo inakuwa kwa maslahi ya vizazi vijavyo.”amesema Ndejembi.
Aidha amewakaribisha wadau wa sekta binafsi kuweza kushirikiana na serikali kwani kushirikiana kwa pamoja kutapelekea wananchi kuwa na makazi bora ya kisasa,kwani serikali ya awamu ya sita inafanya mambo mengi katika kuhakikisha kuwa wananchi wanapata nyumba za bei nafuu kwa watanzania walio wengi.
Naye Rais wa chama cha wataalam wa Miliki Tanzania (AREPTA) Andrew Peter Kato amesema ni mkutano wa Mwaka ambapo wamekutana wataalam tofauti wakiwemo Maafisa Ardhi ,Wathamini,Wataalam wanaofanya uchambuzi yakinifu wa miradi ya Miliki,kwa pamoja watajadili na kufanya uwasilishaji wa kuhusiana na matokeo chanya ya yanayotokana na uboreshaji wa miundombinu Afrika ya Mashariki
Kato amesema wameshirikiana na Jumuiya ya Wataalam wa miliki Afrika ,kwa upande wa Afrika ya mashariki(AfRES) .ambapo wanaongozwa na kaulimbiu isemayo ‘’Uboreshaji wa miundombinu,ya usafiri katika miliki/katika kuongeza thamani ya ardhi Afrika ya Mashariki’’ ,ambapo wanaangazia zaidi katika uboreshaji wa miundombinu haswa mabasi yaendayokasi na Reli katika kuongeza thamani ya ardhi.
Amesema kwa ngazi ya Halmashauri wanachama wao ni wathamini wanaothamini mali wanaponunua nyumba au kufanya uaulishaji kutoka miliki moja kwenda nyingine ili ifanyiwe uthaminishaji ,au kulipa kodi ya ardhi lazima mthamini athaminishe,vilevile kuweka bima lazima mthamini athaminishe mali au mtu anapohitaji kuchukua mkopo.
“Ikumbukwe kuwa hivi karibuni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan alisema kuwa SERA ya Taifa ya Ardhi ya Mwaka 1995 Toleo la Mwaka 2023 iliyozinduliwa machi 17,2025 Jijini Dodoma ina lengo la kuhakikisha nchi inakuwa na mfumo wa umiliki ,upatikanaji na usimamizi wa matumizi ya ardhi kwa maendeleo endelevu na haijabadilika.”amesema Kato.
Akiwasilisha mada kwenye mkutano huo ,Mtaalam wa Ardhi na nyumba ,Mstaafu wa chuo cha ardhi Prof.Joseph Lussuga Kironde amesema kuwa ,shirika la kwanza kuanzishwa lilikuwa shirika la nyumba la Taifa ambapo ulififia miaka ya 1990 na serikali kuhamia zaidi kwenye masuala ya viwanja,ambapo viwanja vikawa havitoshi watu wakawa wanajijenge kiholela .
Hata hivyo amesema kuwa ,Kukosekana kwa sera ya nyumba ya Taifa kumeelezwa kuwa ni mojawapo ya sababu ya kukosekana kwa thamani halisi ya ya miliki ya makazi na biashara,na kuchangia ujenzi holela na makazi duni katika maeneo mbalimbali nchini.
‘’Kwa mawazo yangu hili la watu kujijengea huenda limeondoa ule msukumo wa kwa watu,lakini ukiangalia nyumba walizojenga nyingi hazijaisha zinakuwa kama nyumba zetu ni working progress unajengawee hadi utakapochoka na zipo katika maeneo ambayo hayajapimwa,Ndiyo maana tunasema kwamba nchi inahitaji SERA YA NYUMBA,Kwani sera zinakuja na sharia zake na mipangilio yake na sera hii ikiwemo itatusaidia sana,napendekeza kwamba suala la nyumba liwe kwenye Vision ya Taifa .”amesema Prof. Kironde.