Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Deogratius Ndejembi, akihitimisha Kikao cha Baraza la Wafanyakazi la Wizara hiyo kilichofanyika jijini Dodoma.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Deogratius Ndejembi,akizungumza wakati akihitimisha Kikao cha Baraza la Wafanyakazi la Wizara hiyo kilichofanyika jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhandisi Anthony Sanga akizungumza kwenye Kikao cha Baraza la Wafanyakazi la Wizara hiyo kilichofanyika jijini Dodoma.
Washiriki kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Kikao cha Baraza la Wafanyakazi la Wizara hiyo kilichofanyika jijini Dodoma.
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuhitimisha Kikao cha Baraza la Wafanyakazi la Wizara hiyo kilichofanyika jijini Dodoma.
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuhitimisha Kikao cha Baraza la Wafanyakazi la Wizara hiyo kilichofanyika jijini Dodoma.
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Deogratius Ndejembi amewataka watumishi wa sekta ya ardhi kujitahidi kuwa na usiri kwa kuwa kumekuwa na changamoto kubwa ya usiri ndani ya wizara hiyo.
Waziri Ndejembi amesema hayo wakati akifungua Kikao cha Baraza la Wafanyakazi la Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kilichofanyika jijini Dodoma.
“Jambo linaweza kuwa dogo (Pre mature), lilizungumzwa tu halijafanyiwa hata maamuzi tayari unalikuta liko nje, jambo linaweza likawa pengine ni utekelezaji wa maelekezo mbalimbali pengine ya Serikali lakini unakuta tayari lipo nje, tuna changamoto kubwa sana ya usiri,”amesema
Aidha, Waziri Ndejembi amewataka watumishi wa sekta ya ardhi nchini kutokuwa na woga wakati wa kutekeleza majukumu yao ya kila siku.
“Msiwe waoga katika kufanya maamuzi, usiwe muoga katika kutekeleza majukumu yako na sisi huku juu hata wakati unatekeleza majukumu umefuata sheria na taratibu you are safe” amesema.
Pia, ametumia wasaha huo kuwatakia kila rakheli watumishi wa Wizara hiyo watokwenda kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi ujao wa Oktoba mwaka huu 2025.
Awali Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhandisi Anthony Sanga amehimiza elimu kutolewa kwa wananchi ili waone urahisi wa kutumia mifumo ya kidigiti katika kupata huduma za sekta ya ardhi.
“Wizara kwa sasa iko katika mchakato wa kuwa na Ardhi App itakayo wasaidia wananchi kupakua (download) katika simu zao za mkononi kupata huduma badala ya kutumia tovuti.
“Tayari tushamuelekeza Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA aandae “Ardhi App” ili watu wakidownload ile ‘Ardhi App’ kwenye simu zao za mkononi waweze kuingia na kufanya kazi katika mifumo kupitia simu za mkononi” amesema.