MKUU wa Mkoa wa Dodoma,Mhe.Rosemary Senyamule,akikagua mabanda mbalimbali wakati wa uzinduzi wa maonyesho ya maadhimisho ya siku ya nyuki duniani yanayofanyika katika Viwanja vya Chinangali Park,jijini Dodoma leo Mei 18,2025.

MKUU wa Mkoa wa Dodoma,Mhe.Rosemary Senyamule,akizungumza leo Mei 18,2025 na wananchi wa Mkoa wa Dodoma wakati akizindua maonyesho ya maadhimisho ya siku ya nyuki duniani yanayofanyika katika Viwanja vya Chinangali Park,jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii anayeshughulikia Maliasili, Kamishna wa Polisi Benedict Wakulyamba,akizungumza wakati wa uzinduzi wa maonyesho ya maadhimisho ya siku ya nyuki duniani yanayofanyika katika Viwanja vya Chinangali Park,jijini Dodoma.
SEHEMU ya Wananchi wakisikiliza hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Mhe.Rosemary Senyamule (hayupo pichani) ,akizungumza wakati akizindua maonyesho ya maadhimisho ya siku ya nyuki duniani yanayofanyika katika Viwanja vya Chinangali Park,jijini Dodoma.
Na.Alex Sonna-DODOMA
MKUU wa Mkoa wa Dodoma,Mhe.Rosemary Senyamule,amezindua maonyesho ya maadhimisho ya siku ya nyuki duniani huku akisisitiza ulinzi wa maeneo ya misitu ili kulinda viumbe hai ikiwemo nyuki kwa sababu wana manufaa makubwa kwa Taifa.
Akizungumza leo Mei 18,2025 mara baada ya kuzindua maadhimisho hayo yanayofanyika katika Viwanja vya Chinangali Park,jijini Dodoma Mhe.Senyamule amesema kuwa sekta ya nyuki inakabiliwa na changamoto ambazo zinatishia uendelevu sekta hiyo na hivyo kuhatarisha uvunaji wa mazao ya nyuki kwa siku zijazo.
“Bado tunayo nafasi kubwa ya kukuza na kuendeleza sekta hii. Ni wazi bado tunayo nafasi ya kuhifadhi misitu katika ardhi za vijiji, halmashauri, Serikali Kuu na hifadhi za wanyamapori,”amesema Mhe.Senyamule
Hata hivyo amesema kuwa uchomaji wa misitu ambayo inafanya nyuki kuhama kutoka eneo moja kwenda jingine na wakati mwingine inasababisha kuwapoteza iwapo wataungua na moto huo.