*Mweyenyekiti wa CCM Wilaya ya Kigamboni ampa kongole Diwani kwa kutekeleza Ilani.
Na Chalila Kibuda,Michuzi TV
Diwani wa Kata ya Kibada Amin Sambo amesema kuwa Kibada imepata maendeleo makubwa chini ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan katika kutekeleza Ilani ya CCM katika Kata ya Kibada.
Diwani Sambo aliyasema wakati wa Mkutano wa viongozi wa Matawi na Wanachama wenye lengo la kuonyesha utekelezaji wa miradi mbalimbali katika Kata ya Kibada.
Sambo amesema miradi iliyotekelezwa ni ujenzi wa Vyumba vya madarasa 15 na Matundu vyoo 40 kwa Shule za Msingi na Sekondari kwa ajili ya kufanya wanafunzi wote wanakuwa na madarasa ya kutosha pamoja na vyoo.
Aidha amesema katika jitihada hizo zimefanyika kwa kushirikiana na viongozi vitongoji kwa ufatliaji wa kamati mbalimbali katika miradi yote iliyofanyika katika Kata ya Kibada.
Hata hivyo katika utekelezaji huo ni pamoja na kujenga soko la kisasa ambalo limekamilika na changamoto zake zimetolewa fedha zingine sh. milioni 380 kutatua changamoto hizo zilijitokeza baada ya kukamilika.
Hata hivyo amesema kuwa mradi mwingine ni ujenzi wa Barabara Kilomita 11.3 za DMP pamoja na kilomita 1.3 za barabara kwa fedha za ndani na kufanya Kibada kuwa na muunganiko wa barabara zitazochochea shughuli za kiuchumi kwa wananchi.
Sambo amesema kuwa katika kipindi hiki wananchi na wanacha kuhakikisha wanafanya uhakiki wa daftari la mpiga kura katika kujihakikishia wanapiga kura kwa miaka mitano mingine.
Nae Mwenyekiti wa CCM Wilaya Kigamboni Yahya Sikunjema amesema kuwa Diwani ameweza kutekeleza ilani ya CCM 2020/2025 kwa asilimia 100.
Sikunjema amesema kazi Diwani ni kuwaletea wananchi maendeleo ambapo Diwani wa Kibada ametimiza wajibu huo.
Mwenyekiti wa UWT Kata ya Kibada Mboni Mbegu amesema kuwa kazi yao ni kutaka viongozi wanafanya kazi ambapo diwani wa Kibada amefanya kazi yake kwa weledi katika kutekeleza ilani.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Nazar Kirama amesema kuwa uongozi mzuri ni ule kushiriakiana na kuonyesha kinachofanyika ambapo diwani Sambo amefanya hivyo.
