Kamishna wa Uhifadhi Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania Musa Nassoro Kuji akiwa amesimama baada ya kutambulishwa na Mhe. Dkt. Tulia Ackson Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Mei 19, 2025 katika Ukumbi wa Bunge jijini Dodoma alipohudhuria uwasilishwaji wa Bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii kwa mwaka wa fedha 2025/2026.
Katika uwasilishwaji wa bajeti hiyo Kamishna Kuji ameongozana na Makamanda wa Kanda nne pamoja na Makamishna wengine Waandamizi wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA).