Press Release – Swah
Dar es Salaam, Mei 2025 – Itel Tanzania, chapa ya simu za mkononi zinazotuambulika duniani imezindua toleo jipya la simu yake aina ya Itel A90, kupitia ushirikiano wake endelevu na Airtel Tanzania.
Simu hiyo yenye uwezo na ufanisi mkubwa inawaletea wapenzi wa simu za mkononi uzoefu pekee kwa kidijitali utakaochagizwa na mtandao imara wa Airtel Tanzania na kuhuisha malengo yanayofanana ya Airtel Tanzania na Itel ya kuchochea mabadiliko ya kidijitali kwa kuleta simu zilisheheni thamani na ubunifu mkubwa kwa ajili ya watu wengi zaidi kwa bei nafuu.
Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa simu hiyo, Meneja wa Vifaa vya Intaneti wa Airtel Tanzania, Asnath Mboya, alisema, “Simu ya itel A90 ni hatua kubwa ndani ya ushirikiano wetu na itel katika kuleta suluhisho za kidijitali zenye ubora wa hali ya juu na nafuu kwa ajili ya watanzania. Uzinduzi huu unaakisi malengo ya pamoja ya kuziba ufa wa kidijitali na kuisaidia Tanzania kufikia maono yake ya kuwa na uchumi kamili wa kidijitali. Kwa kuunganisha vifaa vya kibunifu vya itel pamoja na mtandao imara wa Airtel Tanzania wa 4G, tunaenda kurahisisha upatikanaji wa mtandao kwa kila mtu.”
Aliongeza kuwa wateja ambao watanunua simu hiyo wataweza kufurahia data maalum kupitia ofa ya GB75 ili kutajirisha matumizi yao ya simu janja.
Kwa upande wake, Meneja Masoko wa itel Tanzania, Sophia Almeida, alieleza furaha yake kuhusu toleo hilo la simu, “A90 inaendeleza maono yetu ya kutengeneza simu zenye ufanisi mkubwa na muundo wa kipekee. Simu hii inasifa za hali ya juu ikiwemo, betri yenye uwezo mkubwa, ulinzi dhidi ya vumbi na madhara mengine pamoja. Tunajivunia kuendelea kushirikiana na Airtel Tanzania kuwawezesha watu wengi zaid kupitia teknolojia.
Simu hiyo inakioo cha kuonyesha maudhui chenye ukubwa wa nchi 6.56 cha picha ya hali ya juu (HD) na ufanisi 90Hz na ulinzi wa kiwango cha IP54 na muundo ambao unairuhusu kufanya kazi katika mazingira yoyote.
Itel A90 inatumia betri yenye uwezo wa 5000mAh yenye mfumo wa kuchaji wa 15w Type C ili kuwawezesha wateja waendelee kuwasiliana kwa muda mrefu na kuchaji fasta. Pia ina camera ya nyuma nyenye uwezo wa 13mp na 5mp kwa ajili ya Camera ya mbele pamoja na taa inayofanya simu hiyo iwe na picha nzuri ambayo kila mtu anahitaji.
Kupitia uwezo wa uhifadhi GB256 na teknolojia ya memory fusion, A90 inampa mteja uwezo wa kufanya kazi nyingi kwa wakati mmoja kwa wepesi huku nafasi ya kutosha ikibaki kwa ajili ya programu za simu, picha na video. Aidha simu hiyo ina ulinzi wa alama ya kidole na mfumo wa utambuzi sura kwa usalama na wepesi wa kuitumia.