Kamishna wa Uhifadhi – TANAPA Musa Nassoro Kuji akiteta na kufurahia jambo na Mzee Peter Mavunde Meya Mstassvgwa jiji la Dodoma (CCM), wakati walipohudhuria kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Nyuki Duniani yaliyofanyika katika Viwanja vya Chinangali vilivyopo jijini Dodoma jana Mei 20, 2025.
Aidha, Maadhimisho hayo pia yamehudhiriwa na Naibu Kamishna wa Uhifadhi na Maendeleo ya Biashara Massana Mwishawa, Makamanda wa Kanda za Kusini, Mashariki, Kaskazini na Magharibi sanjari na Makamishna, Maafisa Waandamizi pamoja na askari kutoka Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania ambao wamepewa dhamana ya kusimamia na kuendeleza maliasili zote zilizopo katika hifadhi hizo 21 zilizoenea katika mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara.