Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Cyprian Luhemeja amekutana na kufanya mazungumzo na Mabalozi wa Mazingira Mei 20, 2025 katika ukumbi wa mikutano uliopo Ofisi za Makamu wa Rais katika Mji wa Serikali Mtumba, Dodoma.

Mabalozi wa Mazingira wakifuatilia kikao kilichoongozwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Cyprian Luhemeja (hayupo pichani) kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano uliopo Ofisi za Makamu wa Rais katika Mji wa Serikali Mtumba, Dodoma.
…..
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Cyprian Luhemeja amekutana na kufanya mazungumzo na Mabalozi wa Mazingira Mei 20, 2025 katika ukumbi wa mikutano uliopo Ofisi za Makamu wa Rais katika Mji wa Serikali Mtumba, Dodoma.
Akizungumza na mabalozi hao, Mhandisi Luhemeja amewapongeza kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kuunga mkono Serikali katika jitihada za kuhifadhi na kutunza mazingira hususan katika zoezi la upandaji wa miti.
Amesema kuwa mazingira ni suala mtambuka hivyo amewashauri mabalozi hao kutumia fursa zilizopo katika mazingira kwa kupanua wigo wa kushiriki katika utunzaji wa mazingira kwa kutumia fursa zilizopo katika sekta hiyo kwa kuwekeza.
Aidha, Mhandisi Luhemeja ameeleza kuwa ili kuhakikisha suala la mazingira linagusa nchi nzima, Ofisi ya Makamu wa Rais iliwateua Maafisa Viungo wa Mazingira katika mikoa yote 26 ya Tanzania Bara ambao hufanya kazi kwa ukaribu na Maafisa Mazingira wa Mikoa pamoja na Makatibu Tawala.
“Nichukue nafasi hii kuwashauri mjipange ili kila mkoa uwe na Balozi wa Mazingira ambaye atafanya kazi kwa ukaribu na Afisa kiungo pamoja na Afisa Mazingira wa mkoa husika na kwa kufanya hivyo mtaibua fursa nyingi za mazingira na hivyo kujipatia Kipato.
“Halmashauri nyingi sasa zinataka kujiunga na Biashara ya Kaboni, hivyo mkijipanga kimkoa na kwa kushirikiana na Maafisa Viungo na Maafisa Mazingira wa Mikoa mnaweza kuingia kwenye fursa hizo,” alisema.
Pia, Mhandisi Luhemeja alitaja fursa zingine kama upandaji wa miti pembeni ya Bomba la Mafuta pamoja na Reli ya Kisasa (SGR) kwakuwa umbali wa mita 60 kando ya miundominu hiyo unaruhisiwa kupanda miti.
Kwa upande wa mabalozi hao akiwemo Bw. Richard Kalongola alieleza kuwa kutokana na uzoefu wake wa masuala ya maji na gukwe (diving) amenuia kujikita zaidi katika Uchumi wa Buluu wakati Dkt. Margaret Mutaleba ambaye alijitambulisha kuwa ndiye aliyetoa wazo la usafi wa majiji kila Jumamosi alisema amepanga kujihusisha zaidi na usafi wa majiji.
Hivyo, mabalozi hao kwa umoja wao wamemshukuru Katibu Mkuu Luhemeja kwa kutambua umuhimu na mchango wao katika kuhifadhi na kulinda mazingira na kuahidi kufanya kazi kwa ushirikiano mkubwa na Ofisi hiyo ili kuhakikisha mazingira yanakuwa endelevu.