Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Dodoma SACP George Katabazi akizungumza na waandishi wa Habari.







Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Dodoma ( SACP) George Katabazi, akionesha baadhi ya vitu walivyokamata.
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
Jeshi la polisi mkoa wa Dodoma limesema linawashikilia watuhumiwa wanne kwa kosa la kupatikana na silaha bila kuwa na kibali katika wilaya ya Dodoma mjini na Mpwapwa.
Hayo yameelezwa Jijini Dodoma na Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Dodoma ( SACP) George Katabazi wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema watuhumiwa wawili walikamatwa Mei 17.2025 katika mtaa wa Kikuyu mission jijini Dodoma wakiwa na bastola yenye risasi 13.
Kamanda Katabazi amesema watumiwa wengine wawili walikamatwa Mei 19.2025 katika mtaa wa Lukole wilaya ya Mpwapwa wakiwa na risasi tano pamoja na silaha iliyotengenezwa kienyeji na kutumia risasi za shortgun huku ikiwa imekatwa mtutu na kitako chake.
“Jeshi la polisi mkoa wa Dodoma linawashikilia watuhiwa wanne kwa kosa la kupatikana na silaha bila kuwa na kibali katika wilaya ya dodoma mjini na mpwapwa,mei 17.2025 majira ya saa kumi kamili jioni katika mtaa wa kikuyu mission walikamatwa watuhiwa wawili wote wakazi wa Kikuyu mission wakiwa na bastola yenye rangi nyeusi ikiwa na risasi 13 kwenye magazine yake.
“Pia mei 19,2025 majira ya saa kumi na moja kamili jioni katika mtaa wa Lukole wilaya ya mpwapwa walikamatwa watuhiwa wawili wakiwa na silaha iliyotengenezwa kienyeji inayotumia risasi za shortgun iliyokatwa mtutu na kitako pamoja na risasi tano,”amesema.
Aidha amesema wanamshikilia Nestory Kimaro ( 38) na Thomas Paschal maarufu Sigan ( 29) wakazi wa mbabala wakiwa na mafuta lita 2420 aina ya diseli yakiwa kwenye madumu 89 huku yakihifadhiwa katika gari aina ya Toyota Hiace yenye usajili Na: T 273 BKB.
Katika hatua nyingine Kamanda katabazi amesema kufuatia doria iliyofanywa na jeshi hilo limebahatika kukamata vifaa mbalimbali vya kuvunjia,TV 6Redio 7 zinazo dhaniwa kuwa mali za wizi huku watuhiwa 57 wa makisa ya wizi na uvunjaji wanashikiriwa na jeshi hilo ambapo watuhiwa 30 wamefikishwa mahakamani na wengine 27 uchunguzi unaendelea.
Hata hivyo jeshi la polisi mkoa wa Dodoma linatoa wito kwawananchi wanaomiliki silaha kufuata taratibu za umuliki halali wa silaha ikiwa pamoja na usalimishaji wa silaha hizo.