Rais wa zamani wa Jamhuri ya Afrika Kusini Mheshimiwa Thabo Mbeki amewasili Morogoro kwa ziara maalum kutembelea eneo la kihistoria la Mazimbu, ambalo lilikua makazi ya wapigania uhuru wa Afrika Kusini waliokuwa uhamishoni wakati wa utawala wa ubaguzi wa rangi.
Rais Mstaafu Thabo Mbeki amepanda Treni ya SGR kwa ajili ya kwenda Kutembelea Eneo la Mazimbu, Morogoro
Katika Stesheni ya SGR ya Jakaya Kikwete Morogoro Mheshimiwa Mbeki amelakiwa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Malima na viongozi wengine wa Serikali
Ziara hii ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Afrika, yanayoadhimishwa kila mwaka tarehe 25 Mei, ikiwa ni kumbukumbu ya kuanzishwa kwa Umoja wa Afrika (zamani OAU) na kuhamasisha mshikamano, maendeleo na utambulisho wa bara la Afrika.
Mheshimiwa Mbeki yuko nchini kwa mwaliko wa Taasisi ya Thabo Mbeki kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali za Tanzania, ambapo pamoja wameandaa maadhimisho haya ya kitaifa ya Siku ya Afrika.