Mkurugenzi wa KKF,Dominic Shoo akizungumza na waandishi wa hahari jijini Arusha kuhusu maonesho hayo.

Mkuu wa kitengo cha Mauzo na Masoko kutoka kampuni ya Media works Limited, Noel Petro akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maonesho hayo.



Wadau mbalimbali wakiwa katika kikao hicho jijini Arusha.
……….
Happy Lazaro, Arusha
Zaidi ya waoneshaji 500 kutoka nchi 13, mawakala wa usafiri zaidi ya 800 kutoka nchi 40+, na wageni wapatao 15,000 wanatarajiwa kuhudhuria maonesho makubwa ya utalii mashariki mwa Afrika Karibu -Kilifair 2025 yatakayofanyika jijini Arusha juni 6 hadi 8 mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha ,Mkurugenzi wa KKF,Dominic Shoo amesema, “KARIBU-KILIFAIR ni jukwaa kuu kwa waoneshaji zaidi ya 500 kuonyesha bidhaa zao.”.
Shoo amesema kuwa,KARIBU-KILIFAIR ni tukio kuu la utalii Afrika Mashariki na ni matokeo ya kuunganishwa kwa maonesho mawili makubwa ya utalii nchini Tanzania.
“Mwaka huu tumepanua eneo la maonesho kufikia mita za mraba 40,000 katika viwanja vya Magereza, Arusha,Kwa kuzingatia viwango vya kimataifa, ubunifu mpya na mpangilio wa wazi, KKF imejijengea heshima kubwa kama jukwaa bora la biashara ya utalii.”amesema Shoo.
“Hili linathibitisha kuwa KARIBU-KILIFAIR ni tukio kubwa na muhimu zaidi la utalii Kusini mwa Jangwa la Sahara.”amesema Shoo.
Shoo amesema kuwa ,Kampuni ya KILIFAIR Promotion Company Ltd inazindua toleo la 10 la maonesho ya utalii ya KARIBU-KILIFAIR (KKF) ambapo amesema maonesho ya mwaka huu yana utofauti mkubwa kwani yameboreshwa kwa kiwango kikubwa sana .
” Tumepanua eneo la maonesho kufikia mita za mraba 40,000 katika viwanja vya Magereza, Arusha,kwa kuzingatia viwango vya kimataifa, ubunifu mpya na mpangilio wa wazi, KKF imejijengea heshima kubwa kama jukwaa bora la biashara ya utalii.”amesema Shoo.
Kuanzia mwaka huu, tumeanzisha “Jumba la Afrika Mashariki” chini ya mwamvuli wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na kampeni mpya ya “Visit East Africa – Feel the Vibe”.
Kwa upande wake ,Mkurugenzi Mtendaji KKF,Tom Kunkler amesema kuwa,maonesho ya mwaka huu yamelenga utalii endelevu ndani ya Karibu -Kilifair ambapo kwa kulenga mustakabali wa mazingira, wameanzisha mpango wa “Uendelevu wa Utalii” kwa kutumia vifaa vya mbao, vibuyu vya maji, utenganishaji wa taka na maeneo ya kuchakata chupa. Haya ni baadhi tu ya hatua kuelekea maonesho ya kijani ya siku zijazo.
Amesema kauli mbiu ya mwaka huu ni “Biashara hukutana na Wanyamapori” inathibitisha kuwa Tanzania ni kituo bora cha MICE (Mikutano, Maonyesho, Mikutano ya Kitaaluma, na Matukio) ambako biashara na burudani vinakutana.”.
“Serikali ya Tanzania inayoongozwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan imeipa kipaumbele sekta ya utalii. Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Pindi H. Chana, amekuwa akitangaza vivutio vya Tanzania duniani kote,Serikali imeitambua rasmi KARIBU-KILIFAIR kama jukwaa muhimu la masoko ya utalii kupitia pia matukio kama “My Tanzania Roadshows” na “Z-Summit” ya Zanzibar.”amesema .
Tom amesema kiingilio kwa watu wazima ni shs 10,000 kwa watu wazima na 5,000 kwa watoto hivyo ametoa wito kwa wadau mbalimbali kujitokeza kwa wingi kuja kujionea vitu vya tofauti katika maonesho hayo .”amesema.
Mkuu wa kitengo cha Mauzo na Masoko kutoka kampuni ya Media works Limited, Noel Petro, inayoshughulika na machapisho, sare za wafanyakazi, mabango, matangazo, vipeperushi, kudarizi nguo na kuandaa matamasha,alisema kampuni hiyo ambayo inadhamini maonesho hayo imejipanga kwa huduma za tofauti mwaka huu ili kuhakikisha wateja wa utalii wananufaika na huduma hizo.
Amesema pamoja na mambo mengine alisema Kampuni hiyo imejipanga kutoa huduma za machapisho mbalimbali ya utalii zikiwemo tisheti, mashati na mavazi mbalimbali yakuvutia utalii na watalii hapa nchini.
“Kwa wale wenye mabanda katika maonesho hayo ya Kilifair tutatoa huduma ya Kapeti, viti, kuchapisha vipeperushi na mabango” amesema Petro .
Petro ameiomba serikali kuona umuhimu wa waoneshaji kuwa na mabanda ya kudumu na kugeuza eneo hilo kuwa eneo la utalii kuliko kusubiri maonesho ya msimu yanayofanyika kwa mwaka mara moja.