* Kampuni ya Umma Yaweka Msingi wa Kijamii Katika Ikolojia na Uendelevu
KATIKA kuendeleza dhamira yake ya muda mrefu ya kuwa kampuni inayowajibika kijamii na kimazingira, Meridianbet, mshirika wa kimkakati wa Golden Matrix Group (NASDAQ: GMGI), imezindua mapinduzi ya kijani kimya kwa kutekeleza zaidi ya miradi 80 ya kijamii katika robo ya kwanza ya mwaka 2025 pekee.
Baada ya kufanikisha karibu miradi 300 ya CSR katika mwaka wa 2024, Meridianbet imeongeza kasi katika mwaka huu mpya, ikilenga sekta za afya, elimu, michezo ya uwajibikaji, ustawi wa jamii — na kwa kiwango kinachozidi kuongezeka, ulinzi wa mazingira.
Fruška Gora: Michezo Yakutana na Uendelevu
Mwaka huu ulianza kwa mafanikio makubwa nchini Serbia, ambapo Meridianbet ilikuwa mdhamini mkuu wa Mashindano ya 32 ya Fruška Gora MTB Marathon. Wafanyakazi wa kampuni na washirika wa kujitolea walishiriki katika operesheni ya kusafisha njia za misitu katika Hifadhi ya Taifa ya Fruška Gora, wakionesha kwamba michezo na ulinzi wa mazingira vinaweza kuenda pamoja.
Tukio hilo, lililoandaliwa kwa ushirikiano na Meridian Foundation, liliibua msisimko mkubwa kuhusu uwajibikaji wa pamoja kwa mazingira.
“Hatua ya leo si ya kuonyesha tu — bali ni thibitisho kuwa matendo madogo yakifanyika kwa pamoja yanaweza kuleta mabadiliko ya kweli,” alisema Jovan Ignjatović, mwakilishi wa Meridian Foundation.
Kutoka Serbia hadi Tanzania: Harakati ya Kimataifa Inazaliwa
Ufanisi wa tukio la Fruška Gora ulienea kwa kasi, na kuhamasisha timu za CSR katika nchi nyingine, zikiwemo Tanzania, Nigeria na Kenya, kuanzisha miradi ya usafi na uelimishaji kuhusu uhifadhi wa mazingira. Kile kilichoanza kama hatua ya ndani sasa ni harakati ya kikanda, inayounganisha jamii, kuboresha mazingira, na kueneza ufahamu wa kiikolojia katika mipaka ya biashara ya Meridianbet.
Epic Trail: Mazingira, Afya, Jamii — na Kuaminiwa kwa Chapa
Moja ya kampeni kubwa za mwaka 2024 ilikuwa ni “Epic Trail“, tukio la michezo lililowaleta pamoja wakimbiaji, waendesha baiskeli na wanajamii kutoka masoko mbalimbali. Kampeni hii haikulenga tu michezo ya afya, bali ilikuza pia ujumuishaji wa kijamii, ushirikiano wa moja kwa moja, na kuijengea chapa imani ya kudumu katika jamii.
Dira ya ESG: Uendelevu Si Tendo Moja, Ni Dira ya Kidunia
Meridianbet na kampuni mama, Golden Matrix Group, wanachukulia uendelevu kama ajenda ya kimataifa ya muda mrefu. Katika miezi ijayo, miradi mpya itazingatia kupunguza utoaji wa gesi chafu, kulinda bioanuwai, kudhibiti taka, na kuhimiza matumizi ya teknolojia bunifu rafiki kwa mazingira.
Uongozi Wenye Uwajibikaji wa Kweli
Kupitia juhudi hizi zote, Meridianbet inaonesha mfano bora wa jinsi kampuni ya michezo ya kubashiri inaweza kuwa mshirika chanya wa maendeleo endelevu ya jamii. Kama sehemu ya kampuni ya umma inayoorodheshwa kwenye soko la hisa la NASDAQ, mikakati hii ni sehemu muhimu ya dira ya ESG ya Golden Matrix Group — ikileta uwiano kati ya ukuaji wa biashara na athari nzuri kwa dunia.
NB: Jisajili na Meridianbet na cheza michezo ya kasino ya mtandaoni upate ushindi kirahisi, Pia ongeza maokoto yako kwa kubashiri michezo mbalimbali yenye ODDS KUBWA. PIGA *149*10# AU tembelea tovuti yao meridianbet.co.tz