Mhe. Balozi Hamad akiwa na Balozi wa Misri.
……………
Mhe. CP (Mst) Hamad Khamis Hamad, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Msumbiji ashiriki kwenye Sherehe za Maadhimisho ya Siku ya Afrika zilizofanyika Jijini Maputo, Msumbiji tarehe 25 Mei, 2025.
Sherehe hizo pia zilihudhuriwa na Viongozi wengine Waandamizi wa Serikali ya Jamhuri ya Msumbiji akiwemo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa nchi hiyo, Mhe. Balozi Maria Manuela dos Santos Lucas na Mabalozi wa Afrika wanaoziwakilisha nchi zao nchini Msumbiji.
Mhe. Balozi Hamad akiwa na Balozi wa Kenya (Kulia) na Rwanda (Kushoto).