Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Samwel Shelukindo ameongoza washiriki wa mbio za Siku ya Afrika zilizofanyika jijini Dar es Salaam .
Mbio hizo maalum zilizokulikana kama “Africa Day Marathon” ziliandaliwa kwa ajili ya kuadhimisha Siku ya Afrika zilianzia katika Kituo cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) na kumaliza hapo.
Katika Mbio hizo Balozi Shelukindo ameshiriki Kilomita 21 na kumaliza, pia kulikuwa na Kilomita 10 na Kilomita 5 zilihusisha Mabalozi , watumishi wa wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, wanachi na wadau mbalimbali wa wizara
Mbio hizo pia zilishirikisha washiriki kutoka Ethiopia zimeandaliwa kwa Ushirikiano wa pamoja kati ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Umoja wa Mabalozi wa Afrika nchini na ufadhili kutoka GSM, Benki ya TCB, Garda world, EFM, Infocus na hospitali ya JKCI
Mbio hizo ziliandaliwa maalum kwa ajili ya kuadhimisha miaka 62 tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU), sasa ukijulikana kama Umoja wa Afrika (AU), ulioanzishwa tarehe 25 Mei 1963.