Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa Takukuru Mkoani Mara, imefanikiwa kudhibiti malipo hewa ya zaidi ya shilingi Milioni 70 ikiwemo Milioni 49 fedha za uhamishaji wa makaburi kwa wananchi wanaopisha upanuzi wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti katika kata ya Nyatwali Wilayani Bunda Mkoani humo.
Mkuu wa Takukuru Mkoani wa Mara Mohamd Sharif akizungumza Mapema Leo amesema fedha hiyo ilikuwa ilipwe kama kifuta machozi kwa wahusika wa makaburi hewa yasiyo na mili ambapo kila kaburi lilipaswa Kulipwa Shilingi laki 400,000.
Shariff alisema katika fedha hizo shilingi Milioni 21 za Mradi wa ujenzi wa hospital ya Halmashauri ya Wilaya ya Bunda inayotekelezwa katika Awamu ya pili fedha hizo zilitengwa kwaajili ya manunuzi ya vifaa vya ujenzi ambavyo Tayari vilishaununiliwa.
Aidha Taasisi hiyo imefatilia Miradi ya Maendeleo 28 yenye thamani ya shilingi Milioni 9 katika Sekta ya Afya Elimu ,Barabara,na Maji katika Miradi hiyo Miradi 12 ilibainika kuwa na dosari na Ushauri ulitolewa.