Katika kuendeleza mahusiano yaliyojengwa kwa muda mrefu, Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo kimeupokea ugeni wa Mabalozi kutoka Mataifa ya Sweden, Finland, Denmark na Norway (Nordic) na kushuhudia shughuli mbalimbali ambazo zinafanyika SUA.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Raphael Chibunda amesema uhusiano kati ya nchi ya Norway na chuo hicho, unazaidi ya miaka 52 muda ambao serikali ilifanya uamuzi wa kuanzisha ufundishaji wa taaluma ya misitu nchini na ndiyo walikuwa watu wa kwanza waliosaidia kuanzisha shahada ya kufundisha masuala ya misitu.
Kuhusu Denmark, amesema walikuwa wa kwanza kusaidia nchi kwenye ujenzi wa Ndaki yao ya Tiba za Wanyama na waliendelea kusaidia kwa kipindi cha mwanzo kwa kuleta walimu kuja kufundisha wanafunzi wao.
‘‘Kwa hiyo tumewashukuru kwamba kwa kipindi chote hicho wamesaidia Chuo chetu kukua ambapo sasa tumesimama wenyewe na hatua kubwa tumepiga kutoka idadi isiyozidi wanafunzi 2000 hadi tulionao takribani 18,000”, alisema. Prof. Chibunda.
Ameongeza kuwa wamezungumza kuhusu kuimarisha uhusiano huo na kwenda kwenye nafasi kubwa zaidi ya kuhusiana ikiwamo kuwa na uwezo wa kubadilishana wanafunzi pamoja na walimu.
Kwa upande wake Balozi wa Denmark nchini Tanzania, Balozi Jesper Kammersgaard, ameeleza kuwa ushirikiano huo umerahisishwa SUA ambapo kuna maendeleo ya kisasa kutoka kwenye Ndaki ya Mifugo na Sayansi za Afya, maendeleo ya kisasa kutoka katika Ndaki ya Misitu, Wanyamapori na Utalii pamoja Ushirika wa wahitimu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUGECO) ambao unasaidia vijana kuendeleza ujuzi hasa katika nyanja ya kilimo.
Katika kuendeleza mahusiano yaliyojengwa kwa muda mrefu, Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo kimeupokea ugeni wa mabalozi kutoka mataifa ya Sweden, Finland, Denmark na Norway (Nordic) na kushuhudia shughuli mbalimbali ambazo zinafanyika SUA.