Baada ya kuanza zoezi la usambazaji wa vyandarua Mkoani Kigoma MSD leo imeendelea na usambazaji wa vyandarua hivyo huku leo hii ikikamilisha kusambaza kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma. Zoezi hilo linatarajia kuhamia Wilaya ya Kibondo na Kakonko.
Hata hivyo, timu ya usambazaji imekutana na changamoto kadhaa ikiwemo Mto Lwiche ambao upo Manispaa ya Kigoma ujiji. Timu ya MSD imepaswa kutumia usafiri wa Boti na pikipiki kufikisha vyandarua takribani 500 kutoka mtaa wa Kanswa kwenda Ng’ambo Mtaa wa Mgumile.
Mwakilishi wa Menejimenti ya MSD (Mkurugenzi wa Ugavi – MSD) Bw. Victor Sungusia amezungumzia zoezi hilo baada kutembelea eneo hilo na kujionea changamoto za usafirishaji. Sungusia amesema Pamoja na changamoto hizi za miundombinu sisi MSD ndio jukumu letu kwani tutatumia aina yeyote ya usafiri kuhakikisha vyandaru hivyo vinawafikia wananchi kwenye maeneo yao ya ugawaji