SHirika la Masoko ya Kariakoo linatarajia kuendesha mnada wa nafasi kwa wafanya biashara wanaotaka sehemu za kufanya biashara soko jipya la kariakoo kwani soko hilo limeshakamilika kwa asilimia 98 ambapo mnada huo utafanyika kupitia mfumo wa TAUS
Hayo yameelezwa leo Jijini Dare es Salaam na Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko ya Kariakoo, CPA Ashiraph Yusuph Abdulkarim wakati akizungumza na waandishi wa habari namna wanavyoendelea kuratibu wafanyabiashara waliokuwepo kurejea kwenye Soko hilo ambapo kwa idadi walikuwa 1520 lakini hadi sasa waliojisajili kwenye mfumo na kujaza fomu ni wafanyabiashara 1159 na kusema kuwa maeneo mengine ya wazi yaliyobaki yatatangazwa Juni 2 kupitia mfumo wa TAUSI ili yapate wapangaji
“Natoa wito kwa wananchi wote taasisi za uma na binafsi kuchangamkia fursa ya kupata maeneo ya kufanya biasha katika soko jipya la kariakoo kwani bado kuna maeneo yawazi yanahitaji kujazwa baada ya kuwa tumewarejesha wale wa awali waliokuwepo”, ametoa rai CPA Abdulkarim
CPA Abdulkarim amesema wafanyabiashara 361 hawajapangiwa maeneo ya biashara kutokana na changamoto mbalimbali ikiwemo idadi ya wafanyabiashara 134 kutokukamilika kwa taarifa zao ambapo ni taarifa za warithi na tofauti ya majina na NIDA/TIN namba.
Pia CPA Abdulkarim amesema wafanyabiashara 8 kutojisajili kwenye mfumo wa TAUSI, wafanyabiashara 19 wenye makampuni/ vikundi hawajakamilisha taarifa zao, wafanyabiashara 102 hawajajitokeza kujaza fomu na wafanyabiashara 98 hawajakamilisha kulipa madeni wanayodaiwa na Shirika.
Ameeleza kwa sasa soko limekamilika ambapo wanamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia zaidi ya shilingi Bilioni 28 zilizofanikisha mradi huu wa kimkakati ili wafanya biashara kuendelea na biashara zao za kujitafutia kipato na kulipa kodi kwa maendeleo ya taifa.
Vile vile CPA Abdulkarim amesema faida zingine za kiuchumi ni kwenda kuongeza upatikanaji wa ajira zaidi ya 4,000 katika Soko la Kariakoo.
CPA Abdulkarim amesema Shirika limepanga maeneo ya biashara kulingana na aina za biashara na upangaji huo umezingatia tofauti ya biashara ya sakafu moja kwenda nyingine.
Amesema Shirika linakamilisha taratibu za kuwarejesha wafanyabiashara katika soko la Kariakoo, ambapo linawarejesha kwa awamu kulingana na maeneo yaliyokamilika pamoja na aina za biashara zinazofanyika katika maeneo hayo.
Amesema Mpangilio wa maeneo ya biashara na viwango vya kodi katika soko la kariakoo vimepangwa kwa mita za mraba kwa kila sakafu ambapo kila sakafu inapungua bei yake kwa kwenda juu na kila sakafu imepangiwa aina tofauti ya biashara.
Amesema soko linalojengwa lina jumla ya sakafu 8 na maneneo 1,357 ikiwemo vizimba 764 katika maeneo 441 na ramps 152
“Sakafu ya chini ya ardhi kuna eneo la maegesho ya magari, maghala na cold room,Sakafu ya ardhi, sakafu ya kwanza na sakafu ya pili kwa ajili ya biashara ya za mazao mabichi.
“Sakafu ya tatu (252), nne (111) na tano (74) Kwa ajili ya wafanyabiashara wa vifungashio, nafaka, viungo vikavu, viuatilifu na pembejeo za kilimo, mizani na cherehani, policlinic, bidhaa za vyakula na tiba mbadala.
“Sakafu ya sita ni kwa ajili ya migahawa ya chakula na vinywaji,Sakafu ya mzunguko wa barabara ya watembea kwa miguu(Ramp areas) ni eneo maalum kwa kuwapanga wafanyabiashara wadogo (machinga)
Hata hivyo amesema soko lililokarabatiwa lina jumla ya maeneo 550 yenye biashara kama Shimoni Cold Rooms, Stoo, na eneo la Wafanyabiashara wa jumla wa matunda.
Sakafu ya chini na sakafu ya kwanza kuna: ATM na Benki; Bucha za Samaki na Nyama; Fremu za wakala; Nguo na viatu; Vifaa vya simu; vitenge na mashuka, huduma za Stationery Bidhaa za Kiasili na maeneo ya Ofisi za kukodi.