Na Sophia Kingimali.
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mohamed Khamis Abdula amesema MKUTANO, Mkuu wa 14 wa Africa wa Utawala wa Mtandao, (AfIGF) umeazimia kuendeleza ushirikiano wa pamoja kukuza matumizi ya mtandao kufikia maeneo ya vijijini ambayo bado yanachangamoto ili kuhakikisha uchumi wa kidijitali unakua.
Hayo aneyasema Mei 31,2025 jijini Dar es salaam wakati akifunga mkutano huo uliowakutanisha wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi.
Amesema mkutano huo umekubaliana kuondoa changamoto za kikanda za mitandao kuwezesha matumizi ya kadi moja ya simu, badala ya kuwa ya kubadilisha kadi unapoingia nchi nyingine.
Amesema mkutano huo ni muhimu katika kuendeleza elimu na maendeleo kuzalisha ajira, hivyo mkutano umedhamilia kuwa na mikakati wa pamoja wa Afrika kukuza matumizi ya mtandao katika ulimwengu wa sasa wa mageuzi ya dijitali.
“Maendeleo ya digital ni muhimu katika kuendeleza utawala bora na kutoa huduma lakini pia kuzalisha fursa”,amesema.
Amesema kuwa digital inaweza kuendeleza na kuleta mageuzi ya maendeleo kujumuisha watu wote.
Kwa upande wake Mratibu wa kitaifa wa jukwaa hilo Dk.Naza Kilama amesema uwepo wa mkutano huo mkubwa uketokana na juhudi za Rais Dk Samia Suluhu Hassan katika kuifungua nchi kimataifa lakini kuruhusu uwekezaji mkubwa nchini.
Aidha amesema kuwa mkutano huo nchini umefanyika kwa ukubwa na umekuwa na fursa mbalimbali lakini umetoa fursa kwa wadau kubadilishana mawazo kwa vitu mbalimbali vinavyofanyika Afrika.
“Katika mkutano huu tumejadiliana namna ya kutumia kadi moja kwa nchi zote za Afrika hii itasaidia kuinua uchumi wa kidigital”,amesema.