NA DENIS MLOWE IRINGA
ORODHA ya timu zilizofudhu hatua ya 16 bora ya kombe la Vunjabei zimejulikana mwishoni mwa wikii baada ya timu ya Kalenga Fc kuifunga wapinzani wao magoli Mgama fc kwa magoli 2 – 1 na katika mchezo uliopigwa uwanja wa Kalenga.
Mashindano hayo yanayofadhaminiwa na kampuni ya Vunjabei chini ya Fred Ngajilo aka Fred Vunjabei aliyeweka milioni 10 kwa bingwa yamekuwa na msisimko mkubwa mkoani hapa kutokana na zawadi kubwa kwa bingwa.
Timu nyingine zlizofankiwa kutinga hatua hiyo ni timu za Morning Fighter Fc , Tanesco fc, Isakalilo fc,Mgela fc, Nzihi fc, Spana Fc, Kidamali fc na BBC fc.
Aidha timu nyingine ni Wasa fc, Mtipesa Fc, Lumuli fc, Viwengi fc , Migori fc, Kising’a Fc , Ifunda Combane fc na Kalenga fc.
Akizungumza na mwanahabari hizi, Katibu wa Mashindano hayo Yahaya Mpelembwa alisema kuwa baada ya kupatikana kwa timu 16 zitakazoenda hatua ya robo fainali wanazipongeza timu zilizofika hatua hii katika kuwania kitita cha milioni 10 na zawadi nyingine nyingi kwa mchezaji bora wa mashidano,mfungaji bora nk.
“Tunaendelea kumshukuru mdhamini kwa kuendelea kuwezesha ligi ichezwe tena kwenye kiwango cha juu kabisa hakika Fred Vunjabei nia mkombozi wa mpira kwani tumeona timu zikicheza kwa kiwango kikubwa kabisa ameleta mapinduzi hasa kwenye zawadi”Alisema
Aliongeza kuwa katika hatua hii wanatoa taarifa kwa timu zilizotinga hatua ya 16 bora kuwa dirisha la usajili limefunguliwa na timu zifanye maandalizi kwa muda wa siku tano baada ya hapo ratiba itatoka kuendelea na hatua hiyo.
Mpelembwa aliwataja vinara wa magoli katika mashindano hayo hadi kupatikana kwa hatua ya 16 bora kuwa ni mchezaji hatari kutoka Isakalilo fc , Barnaba Karlo mwenye magoli 6 akifatiwa kwa ukaribu na Osca Evaristo mwenye magoli 5.
Orodha ya wafungaji wenye magoli manne ni Amasha Mlowosha , Nassoro Chollo na Hosea Kalevela wakati wenye magoli matatu ni Bright Mgoyo, Ernest Nduguru, Fadhili Malenda, Hussein Idd , Choti Mfalingundi na Michae Sadat ambao timu zao zimefanikiwa kufuzu hali ambayo wakitumia vyema wanaweza kuwa vinara.