WAZIRI wa Afya Mhe.Jenista Mhagama,akiwalisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2025-2025 leo Julai 2,2025 bungeni Dodoma.
Na.Alex Sonna_DODOMA
KATIKA mwaka wa fedha 2025-2026 Serikali imetenga Sh bilioni 123.93 kwa ajili kuimarisha huduma za matibabu ya ubingwa na ubingwa bobezi pamoja na kuimarisha tiba utalii nchini.
Hayo yameelezwa leo Julai 2,2025 na Waziri wa Afya,Jenista Mhagama wakati akiwaslisha bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2025-2026.
Waziri Jenista amesema fedha hizo ni kwa ajili ya kuendelea kutoa huduma za matibabu ya ubingwa na ubingwa bobezi katika Hospitali ya Taifa, Hospitali maalum, Hospitali za Rufaa za Kanda na Hospitali za Rufaa za Mikoa pamoja na kuanzisha na kuimarisha huduma mpya kulingana na mahitaji zikiwemo.
Pia,upandikizaji wa ini katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kampasi ya Upanga na Kuanzisha huduma bobezi za mfumo wa mkojo na uzazi kwa wanaume (Uro-andrology) katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kampasi ya Mloganzila.
Vilevile,Kuanzisha upasuaji na ubadilishaji wa mabega na viwiko (Shoulder and Elbow Replacement) katika Taasisi ya Mifupa Muhimbili,Kuendelea kutoa huduma ya upasuaji wa ubongo, uti wa mgongo, nyonga na magoti kwa kutumia mfumo wa 215 akili mnemba katika Taasisi ya Mifupa Muhimbili MOI.
Pia,Kuanzisha huduma ya matibabu ya wagonjwa waliopata kiharusi na mishipa ya damu ndani ya ubongo bila kufungua fuvu (Interventional Neuro-radiology) katika Hospitali ya Benjamin Mkapa.
“Kuanzisha huduma sita za kibingwa kwa fani za Radiolojia, Usingizi, Ngozi, Macho, Magonjwa ya akili na Magonjwa ya Damu Katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Maweni Kigoma.Kuanzisha huduma za kibingwa za upasuaji wa taya na uso (Maxillofacial Surgery) katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Iringa,”amesema Waziri Jenista
Pia, Kuanzisha huduma za kibingwa za masikio, pua na koo katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Kitete (Tabora)
Kuendelea na hatua za awali za utekelezaji wa mradi wa maboresho makubwa ya Hospitali ya Taifa Muhimbili,kuanzisha kiwanda cha kuzalisha viungo tiba na viungo saidizi (Prostheses Manufacturing Plant) katika Hospitali ya Kanda KCMC.
“Kuendeleza na kuimarisha huduma za mkoba za kimkakati za ubingwa na ubingwa bobezi ndani na nje ya nchi (International Medical Camps),”amesema