WAZIRI wa Afya Mhe.Jenista Mhagama,akiwalisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2025-2025 leo Julai 2,2025 bungeni Dodoma.
Na.Alex Sonna_DODOMA
KATIKA Kuimarisha mifumo ya ugharamiaji wa huduma za afya nchini ikiwa ni pamoja na kuendelea na utekelezaji wa Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote, kiasi cha Shilingi Bilioni 49.80 kimetengwa katika bajeti ya mwaka 2025-2026.
Hayo yameelezwa leo Julai 2,2025 na Waziri wa Afya,Jenista Mhagama wakati akiwaslisha bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2025-2026.
Waziri Jenista amesema fedha hizo ni kwa ajili ya kukabiliana na mabadiliko ya Sera yasiyotarajiwa kutoka kwa nchi za magharibi.
Pia Kusimamia utekelezaji wa Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote nchini kwa kuanza kutoa kadi za Bima ya Afya kwa makundi mbalimbali.