*Miradi yote yapitishwa na Mwenge wa Uhuru 2025 hakuna mradi uliokataliwa.
Mwenge wa Uhuru Mkoa wa Dar es Salaam umeanza kukimbizwa katika Wilaya ya Temeke ikiwa ni Wilaya ya kwanza katika Mkoa huo.
Mwenge wa Uhuru katika wilaya hiyo umepitia miradi saba yenya thamani ya *Tsh 17,127,522,627.88* ambayo ni Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha Polisi, Barabara ya Masaki Toangoma, Mradi wa shule ya Sekondari Mangaya-Mbagala, Mradi wa utengenezaji wa mabegi unaotokana na mkopo wa asilimia kumi, Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya Chamazi, Mradi wa shule ya Sekondari Yombo Dovya na mradi wa Nishati safi.
Aidha Mbio za Mwenge wa Uhuru 2025 leo Juni 2, 2025 unaendelea kukimbizwa katika Wilaya ya Kigamboni Mkoa wa Dar es Salaam ambapo utakagua, kuweka jiwe la msingi na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo