WAZIRI wa Afya Mhe.Jenista Mhagama,akiwalisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2025-2025 leo Julai 2,2025 bungeni Dodoma.
Na.Alex Sonna_DODOMA
WIZARA ya Afya imetaja vipaumbele 10 itakavyovitekeleza katika bajeti ya mwaka 2025-2026 ikiwemo Kuimarisha huduma za kinga dhidi ya magonjwa ya kuambukiza yakiwemo magonjwa ya milipuko, magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele, magonjwa yasiyoambukiza na huduma za Lishe.
Akiwalisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2025-2025 leo Julai 2,2025 bungeni,Waziri wa Wizara hiyo,Jenista Mhagama avitaja vipaumbele hivyo ni Kuimarisha upatikanaji na ubora wa huduma za afya zinazotolewa katika ngazi zote kuanzia Zahanati hadi Taifa.
Vipaumbele vingine ni Kuimarisha mifumo ya ugharamiaji wa huduma za afya nchini ikiwa ni pamoja na kuendelea na utekelezaji wa Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote,Kuendelea kufanya tafiti na kuhimiza matumizi ya matokeo ya tafiti hizo kwa maeneo ya kimkakati.
Pia Kuimarisha huduma za afya ya uzazi, mama na mtoto ili kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi na watoto wachanga,Kuimarisha upatikanaji na uendelezaji wa wataalam katika Sekta ya Afya kwa fani za kati, ubingwa na ubingwa bobezi.
Vilevile Kuimarisha huduma za matibabu ya 208 ubingwa na ubingwa bobezi pamoja na kuimarisha tiba utalii nchini,Kuendeleza na kusimamia afua za Tiba Asili na Tiba Mbadala.
Vipaumbele vingine ni Kuimarisha upatikanaji wa huduma za tiba dhidi ya magonjwa ya kuambukiza, magonjwa yasiyoambukiza na magonjwa ya mlipuko na Kuimarisha huduma za afya ya akili, huduma za utengamao hususan kwa watoto, wazee na watu wenye ulemavu.