WAZIRI wa Afya Mhe.Jenista Mhagama,akiwalisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2025-2025 leo Julai 2,2025 bungeni Dodoma.
Na.Alex Sonna _DODOMA
WIZARA ya Afya imeliomba Bunge kuliidhinishia Sh trilioni 1.6 kwa ajili ya kutekeleza vipaumbele 10 katika mwaka wa fedha 2025-2026.
Akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya bajeti hiyo leo Julai 2,2028 bungeni kwa mwaka wa fedha 2025-2026,Waziri wa Wizara hiyo,Jenista Mhagama amesema kati ya fedha hizo sh bilioni 626 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na Sh bilioni 991 ni kwa ajili ya miradi ya maendeleo
Kwa mwaka wa fedha 2025/26, Wizara imepanga kutumia kiasi cha Shilingi bilioni 62.,433. kwa ajili ya matumizi ya kawaida sawa na Asilimia 39 ya bajeti iliyotengwa, ambapo kiasi cha Shilingi 475,418,119,000.00 ni kwa ajili ya Mishahara ya Wizara na Taasisi zilizo chini yake, na kiasi cha Shilingi 151,015,017,000.00 ni kwa ajili ya matumizi mengineyo.