*Miradi yote Wilaya ya Kigamboni yapitishwa na Mwenge wa Uhuru hakuna mradi hata mmoja uliokataliwa.
Mwenge wa Uhuru 2025 unaendelea kukimbizwa katika Mkoa huo ambapo Wilaya ya Kigamboni *miradi 7 yenye thamani 6,743,696,588.37* imepitiwa na Mwenge hakuna mradi uliokataliwa.
Aidha katika miradi hiyo Mwenge wa Uhuru 2025 umetembelea, umekagua, kuweka jiwe la msingi na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo kama, Ujenzi wa barabara ya Rombo Bar RC Church km 0.39 na Kivukoni Shule ya msingi km 0.25, Mradi wa kikundi cha vijana Umoja kwanza, Ujenzi wa Kituo cha Afya Mjimwema, Mradi wa Mazingira, Taka ngumu na Nishati safi, Mradi wa usambazaji wa Maji, Ukarabati na Upanuzi ofisi ya Serikali ya Mtaa Mwera, pamoja na Mradi wa Bweni la wanafunzi shule ya Sekondari Kidete.
Mwenge wa Uhuru 2025 leo Juni 3, 2025 unaendelea Wilaya Ilala ambapo utatembelea, utakagua, kuweka Jiwe la msingi na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo.
*Jitokeze Kushiriki Uchaguzi Mkuu mwaka 2025 kwa Amani na Utulivu