Pembezoni mwa Mkutano huo wa Bodi, Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete alipata pia fursa ya kukutana na kufanya kikao na Waziri anayeshughulikia Ubia wa Kimataifa na Nchi zinazozungumza Kifaransa Thani Mohamed-Soilihi ambapo pamoja na mambo mengine walijadili namna ya kukuza zaidi ushirikiano kati ya Taasisi ya GPE na Ufaransa.




Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza Mkutano wa Bodi ya Taasisi ya Ubia wa Elimu Duniani (Global Partnership for Education – GPE), ambayo yeye ni Mwenyekiti wake, unaofanyika jijini Paris, Ufaransa leo tarehe 3 Juni na kesho 4 Juni, 2025 na kuhuduriwa Wajumbe zaidi ya 40 wanaowakilisha makundi mbalimbali ya Ubia huo ambao wanatoka nchi 7 tajiri zaidi duniani (G7), nchi washirika kutoka kanda zinazoendelea kiuchumi, hususan zilizopo Afrika na Asia, pamoja na Mashirika mbalimbali ya kimataifa.