Kupitia anwani ya www.tausi.tamisemi.go.tz, wafanyabiashara wataweza kuona maeneo yote ya biashara yaliyotangazwa kwa njia ya mnada. Mnada huu wa kielektroniki utafanyika kuanzia tarehe 05 Juni, 2025 saa 1:00 Asubuhi hadi tarehe 11 Juni, 2025 saa 1:00 Asubuhi.
Ili kushiriki, mfanyabiashara anapaswa kujisajili kwenye mfumo wa TAUSI PORTAL akiwa na taarifa zifuatazo:
Namba ya Kitambulisho cha Taifa (NIDA)
Namba ya Mlipa Kodi (TIN)
Barua pepe (Email)
Namba ya simu
Wananchi na wafanyabiashara wote mnaombwa kutumia fursa hii muhimu kwa ushiriki wa haki na uwazi.
Imetolewa na:
Ashraph Y. Abdulkarim
MENEJA MKUU
Shirika la Masoko ya Kariakoo