Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba imekuwa ikifanya vizuri kwa miaka mitatu mfululizo katika matokeo ya mitihani ya shule za Sekondari.
Awamu hii hari imekuwa tofauti kwani Shule za Msingi nao wameitoa Kwi.ba kimasomaso baada ya kushika namba moja kati ya Halmashauri 43 za Mikoa sita ambapo katika madaraja na asilimia Kwimba imeongoza.
Akikabidhi zawadi kwa Walimu wakuu ambao shule zao zimeingia kumi bora katika mtihani wa utamilifu darasa lasaba Mkuu wa Wilaya Mhe. Ng’wilabuzu Ludigija amewapongeza walimu wote kwa kuendelea kujitoa kufundisha na kuiletea heshima Kwimba
“nawapongeza sana walimu wote kwa kuwa wakwanza kwenye haya matokeo endeleeni kuiheshimisha Kwimba kwa kufanya vizuri zaidi, pia niwajulishe tu kuwa hili ni deni haya matokeo tunayatarajia kwenye mtihani wa Taifa” amesema Ludigija
Mkuu huyo amewataka Maafisa Elimu Kata kuongoze usimamizi wa Elimu katika kata zao ili kuhakikisha ufaulu wa wanafunzi unasonga mbele.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Dkt.Amon Mkoga ametumia wasaa huo kuwapongeza walimu kwa kufanya vizuri katika, pia amewaahidi kuwapatia motisha ya kufanya utalii Zanzibari endapo wataendelea kuongeza ufaulu
” nimefurahishwa na taarifa hizi, kwi.ba nayo ijulikane kwa mambo mazuri kama haya” amesema Mkoga
Akuwasilisha taarifa Afisa Elimu Taaluma Mwalimu Simbulya amesema ” jumla ya Halmashauri 43, shule zaidi ya elfu nne Halmashauri imeshika nafasi ya Kwanza katika vigezo vyote vya asilimia na wastani”
Amesisitiza kuwa Halmashauri imekuwa kinara pia katika ufaulu wa masomo ya Hisabati na Kingereza.Katika hafla hiyo vifaa vya ufundishaji vimetolewa kwaajili ya kuboresha ufundishaji na ujifunzaji