Gari mziki iliyokuwa kwenye msafara wa Makamu Mwenyekiti wa Chama Mhe. John Heche imepata ajali alfajiri ya leo maeneo ya Msamvu mkoani Morogoro, wakati inaelekea Kivukoni – Ulanga, Igima – Mlimba, Ifakara Mjini na Kilombero kuanza operesheni #NoReformsNoElection Kanda ya Kati. Gari hiyo ilikuwa inaongozwa na Twaha_Mwaipaya, kuna baadhi ya watu wamepata majeraha na wamepelekwa hospitali ya mkoa Morogoro kwa uangalizi zaidi wa afya zao.