Mkuu wa idara ya masoko wa kampuni  hiyo,Veronica Kibindo akizungumza jijini Arusha leo . 

Mkuu wa idara ya masoko wa kampuni  hiyo,Veronica Kibindo akitoa elimu kwa wataalamu wa mifumo ya Tehama wakati walipotembelea banda lao jijini Arusha leo . 
…………
Happy Lazaro,  Arusha .
Kampuni ya SOFT -TECH CONSULTANTS LTD yenye makao yake makuu jijini Dar es Salaam ni wadhamini wakuu katika mkutano wa Wataalamu wa mifumo ya Tehama unaofanyika jijini Arusha ambapo imekuwa ikiongoza katika utoaji wa huduma za ushauri wa kiteknolojia na suluhisho za biashara .
Aidha kampuni hiyo pia imekuwa ikijishughulisha na  uunganishaji wa mifumo, ikilenga kusaidia makampuni ya Afrika ya Kusini mwa Jangwa la Sahara kuboresha na kukua katika enzi ya kidijitali. 
Mkuu wa idara ya masoko wa kampuni  hiyo,Veronica Kibindo  amesema kuwa,kwa mwaka huu wamekuwa  mmoja wa  wadhamini wakuu wa mkutano wa Jumuiya ya wataalamu wa Teknolojia ambao wanatoka kwenye nyanja mbalimbali ( ISACA)  jambo linalodhihirisha dhamira yao ya dhati ya kuendeleza sekta ya Tehama nchini.
Amesema kuwa wana  matawi katika nchi mbalimbali ikiwa ni pamoja na Uganda, Ghana, Gambia, Lesotho, Zanzibar, Nigeria, Malawi, na India. 
Veronica amesema kuwa,kwa miaka zaidi ya 32 kampuni hiyo imechangia pakubwa katika kuendeleza mifumo ya kidigitali usalama wa taarifa na katika   kutumia teknolojia bora.
Amefafanua  kuwa malengo ya muda mrefu ni kuchangia katika kuandaa mazingira salama ya kuhakikisha kwamba tunajenga Taifa la kisasa lenye misingi imara ya kidigitali. 
“kampuni yetu  inatoa huduma mbalimbali ikiwemo huduma ya usimamizi wa usalama wa  mitandao ,na uchambuzi wa takwimu ,wanatoa huduma ya usimamizi wa  miundombinu katika kituo cha Deita,wanatoa suluhisho katika manunuzi ya kieletroniki ,wanatoa huduma za afya ,pamoja na kutoa huduma za akili bandia n.k “amesema Veronica .
“Najua kuna dhana ya  baadhi ya watu kuogopa kutumia Tehama  lakini niwatoe hofu kuwa kuna umuhimu wa  watu kufahamu matumizi ya Tehama katika kujua mazuri na mabaya yake na hakuna sababu ya kuogopa kutumia Tehama kikubwa ni kujua matumizi ya Tehama mazuri na mabaya ya Tehama na Tehama haipukiki .”amefafanua Veronica .
Ameongeza kuwa,zipo suluhisho  mbalimbali zinazosaidia kuepukana na madhara ya kutumia Tehama ikiwemo suluhisho za usalama wa mitandao ,uchambuzi wa takwimu ,ambapo huduma hizo wanatoa katika kampuni yao .
Aidha amesema kuwa ,kwa kawaida  kuna dhana ya watu  kuogopa mambo mapya yanapotea lakini inafika mahali wanazoea  kwani kadri siku zinavyoendelea kwenda mbele mifumo itakuwa ni moja katika maisha yetu ya kila siku.hivyo haipukiki.








